Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 26, 2013

IBRA DA HUSTLER "MWANAMKE NDIE ALIYENIFANYA NITUMIE MADAWA YA KULEVYA"

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Kenya Ibra Da Hustler akiwa katika pozi.

WAKATI kesho dunia inaadhimisha siku ya matuizi ya dawa za kulevya Rapper Ibra Da Hustler amefunguka kuwa sasa anampango wa kubadilisha maisha yake kwa uamuzi aliouchukuwa wa kuachana na matumizi ya dawa aina ya Herion na Crack Cocaine.

Da Hustler ameamua kuachana na matumizi hayo ya dawa za kulevya baada ya kuona kuwa ni uharibifu wa pesa pili kitendo hicho ni kukaribisha dharau kwenye maisha yake huku akihatarisha maisha, Rapper huyo ambaye kwa sasa ana takribani siku nne hajagusa toka amejiunga na taasisi amejifunza kuvumilia na matumaini yake ni kuachana kabisa na matumizi hayo ya dawa za kulevya.

Akizungumza na habarimpya.com alisema kwamba mwanamke ndiye aliyemshawishi mpaka akiingiza katika matumizi ya dawa ya kulevya. “Kuna binti alinishawis kutumia dawa na ndio nikajikuta nimeingia katika mkumbo huu najuta kumfahamu nakubaini kuwa hataki maendeleo yangu kabisa nanimejifunza kutoka kwake, sasa nikimwambia mtu usiguse dawa ataamini kwani najua kitu gani atapata kwenye maisha yake”alisema Dar Hustler.
 

No comments:

Post a Comment