Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 14, 2013

>LADY JAY DEE AFUNGUKA. WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA


Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri
hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye
maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na
mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu
zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na
watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na
hata wenye ukubwa wa connection katika hii
industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani
lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha
nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi
iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua
kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na
misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija
unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka
kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna
msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu
mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu
niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya
mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na
kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana
jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu
cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu
hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza
kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza
sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu
mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia
asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM
isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote
kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie
msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa
marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu
yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao
wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya
biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri
nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi
haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili
ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini
ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini
naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa
mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi
kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba
dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi
nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua
kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita
njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna
watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond
ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya
nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne
mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii
wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo
hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu
nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja
nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila
yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni
mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide
inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

No comments:

Post a Comment