Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 11, 2013

Matusi ya Kagame kwa Rais Kikwete yawagawa watanzania

Dar es Salaam,Tanzania
MATUSI ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete yamewagawa Watanzania.
Rais Kagame alimtukana Rais Kiwete kwa kuita ushauri wake kwamba ni ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa,awali Rais Kikwete alizishauri nchi za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.

 RAIS KAGAME AKISISITIZA JAMBO

“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais Kagame.
Katika hatua nyingine Rai Kagame alisema kwamba ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea wanyarandwa mbele ya mataifa. Rais Kagame aliyasema hayo katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya maofisa wa jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo ya kijeshi siku ya Juma Tatu nchini Rwanda.
Ingawa haijajulikana mara moja kwamba baadhi ya watu walioandika maoni yao katika mtandao wa Facebook ni watanzania ama baadhi yao si watanzania, huku wakidai kwamba Rais Kagame yuko sahihi
YOU MIGHT ALSO LIKE THIS

No comments:

Post a Comment