Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 22, 2013

UPDATE:: MWANAFUNZI WA UDSM ALIYEPIGWA RISASI YA TUMBO NA MAJAMBAZI AFARIKI DUNIA ...!

HABARI zilizotufikia hivi Punde zinasema kwamba mwanafunzi ALEX ROBERT wa chuo kikuu DAR ES SALAAM (UDSM) amefariki dunia mchana huu katika HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ambapo alikuwa amelazwa kutokanana kujeruhiwa na risasi ambyo alipigwa na majambazi walimvamia akiwemo yeye pamoja na wenzake watatu.
Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani walivamiwa na majambazi usiku wa kuamkia jana maeneo ya Yombo chuoni hapo. Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA KIJANA ALEX ROBERT.. AMINA

No comments:

Post a Comment