Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 12, 2013

AGNESS MASOGANGE AKIRI KUWEKWA LUPANGO SOUTH AFRIKA

HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi.
Kwa mujibu wa habari ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”
 

KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea. 

Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.
Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.     
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”
Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
Habari hii imeandikwa na Imelda Mtema, Haruni Sanchawa na Musa Mateja.

CREDIT:GAZETI LA IJUMAA

No comments:

Post a Comment