Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, July 6, 2013

BASI LA SUMMRY LAPATA AJALI NA KUUA WATU TISA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA...!

Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu.


Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.

Chanzo:  lukwangule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment