Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 7, 2013

HII NDIO HALI HALISI YA SHOW YA KILI MUSIC AWARDS TOUR MJINI MOSHI…!

  
Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni ya kuingia katika uwanja wa ushirika kushuhudia Kili Music Tour.
 Watu wakiwahi nafasi za mbele ili waweze kuona show vizuri na kwa karibu zaidi.
Watu wakiwa wamelizunguka jukwaa la Kili Music Tour wakishuhudia show kutoka kwa wasanii mbalimbali wa hapa Tanzania.

Hapa Dj choka kushoto na Kassim a.k.a Babi D'e Conscious. DJ Somjo kwenye moja na mbili akifanya yake.

Nawapongeza sana waandaji wa mashindano ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards kwa jinsi ambavyo wamekua kichocheo kikubwa cha kukuza mziki wa Tanzania na pia wamekua mfano mzuri wa kuigwa kwa jinsi ambavyo wamekua wakiyaandaa mashindano hayo ambayo ni mashindano makubwa sana na yenye heshima kubwa hapa nchini Tanzania.
Na kila mwaka mashindano haya hufanyika jijini dar es salaam lakini kwa kuwa waandaji wa mashindano haya wanatambua umuhimu mkubwa wa washabiki na wapenzi wa muziki wa Tanzania waliopo mikoani wakaamua kuandaa tamasha ambalo linafahamika kama Kili Music Awards Tour lengo likiwa ni kuzunguka katika mikoa ya Tanzania ili mashabiki walioko mikoani nao wapate burudani kutoka kwa wasanii waliobahatika kupata tuzo na husindikizwa na wasanii ambao pia kwa kipindi hicho wanakua wanafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari.
Kwa mwaka huu pia nazidi kuwapa pongezi katika yale wanayoendelea kuyafanya kwa kuwa kwa wao kuendelea kufanya hivi wanavyofanya naamini ni njia mojawapo ya kukuza mziki wa hapa Tanzania. Tamasha la Kili Music Awards Tour liliyofanyia mjini Moshi mkoani Kilimanjaro usiku wa tarehe 6/07/2013 kuamkia siku ya tarehe 7/07/2013 naweza kusema ni tamasha ambalo limevunja rekodi ya kuwa na watu wengi sana kwa hapa mjini Moshi na ila ni tamasha ambalo halikukosa mapungufu.

        Mazuri:
 • Tamasha hili lilifanyiwa matangazo ya kutosha katika vyombo mbalimbali vya habari na katika mitandao ya kijamii. Matangazo hayo yalifanikisha kwa kiasi kikubwa sana watu wengi sana kuweza kuhudhuria katika tamasha la Kili Music Awards Tour ya mjini Moshi. Na iliweza kuwa na watu zaidi ya elfu tano, wakiwemo watu wazima na watoto, wakazi wa mji wa Moshi na wengine walitokea nje ya mji wa Moshi.
 • Walijitahidi kuweka nyama choma na beer aina ya  Kilimanjaro za kutosha, pia waliweka vinywaji aina ya grand malt na maji kwa wale wasiotumia kilevi. Jukwaa pia liliandaliwa vizuri sana kwa ajili ya wasanii kuweza kufanya show na kila mtu aliyeweza kuingia uwanja wa ushirika aliweza kuona kilichokua kikiendelea pale jukwaani. 
 • Nawapongeza sana wasanii wa kundi la Jambo Squad  (mamong’o) kwa kuweza kutoa burudani kwa mashabiki waliofika katika uwanja wa ushirika. Wasanii wengine waliofanya vizuri ni Lady Jaydee (teamANACONDA), Roma Mkatoliki, Joh Makini, Kala Jeremayah, Diamond na Snura.

       Mapungufu:
 • Watu walikuwa wengi kiasi ambacho tiketi ziliisha na hakukuwa na njia mbadala ya kuweza kuwapatia watu tiketi zaidi ya watu kuwapa walinzi wa mlangoni pesa na kuingia ndani kitu ambacho nadhani kinaweza kuwa kiliwakosesha waandaaji wa tamasha hilo kuzikosa baadhi ya pesa zile zilizoingia kwenye mifuko ya walinzi wa getini.
 • Waliruhusu watoto wenye umri wa chini ya miaka kumi na nane kuingia uwanjani na matokeo yake liliibuka wimbi kubwa sana la watoto waliopotezana na ndugu zao na katikati ya show kulikua na matangazo ya kutangaza watoto waliopotezana na ndugu zao, jambo ambalo halikua sahihi hata kidogo.
 • Waliofunga muziki/speakers hawakua wamejiandaa vya kutosha kwa kuwa speakers zilikua zikikoroma na wakati mwingine zilitoa sauti kali zilizokua zikiumiza masikio. Na wasanii walipokua wakiimba kulikua na tatizo la mziki kuzima mara unarudi tena mara unazima na ilipelekea wasanii wengine kushindwa kufanya vizuri jukwaani.
 • Wasanii wa mjini Moshi hawakupata nafasi hata moja ya kuonyesha vipaji vyao kwenye tamasha kubwa kama hili. Sio kawaida sana kuona tamasha lolote likifanyika mahali popote bila kuwa na wasanii wachanga (undergrounds) wa mji au mkoa husika kupanda jukwaani kuonyesha uwezo wao.
 • Wasanii walioshindwa kufanya vizuri jukwaani ni Barnaba Boy yeye alishindwa kuwasiliana na Dj wake na mashabiki wake pia alionekana kutokua na pumzi na pia kutokujiamini kwa kile alichokua anakifanya jukwaani.
 • Ben Paul yeye alionekana kujiamini katika kuimba lakini hakuweza kuwasiliana na Dj wake na ilimfanya wakati mwingine kuimba na kufikia katikati ya wimbo na kuanza tena kuimba pia hakua amejiandaa na kufanya mazoezi ya kutosha. Japo baadhi ya nyimbo zake zilionekana kuimbwa na mashabiki wakati akiwa jukwaani lakini Ben Paul aliyekua jukwaani sio sawa na yule Ben Paul aliyezoeleka kusikika kwenye radio na kuonekana kwenye TV.
 • Professor Jay alionekana kuwa na mzuka sana lakini kwa kweli kiwango chake kimeshuka na anahitaji mazoezi sana ili kuweza kuwa na pumzi ya kutosha maana tayari ni msanii mkubwa na ni msanii ambaye amekua kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kwa muda mrefu sana na watu wengi walitegemea kuona vitu vipya na vyenye ubunifu wa hali ya juu ili kuweza kuwadhihirishia watu kuwa yeye ni mkongwe na muziki anauweza. Sikutegemea msanii mkubwa kama professor Jay angeweza kupanda jukwaani alafu katikati ya show anaanza kumuita  DJ Choka aje kufanyia back voco.
 • Vyoo navyo havikuwa vimeandaliwa kwaajili ya tamasha kubwa kama hili maana ulifika wakati vyoo vikafurika uchafu kiasi kwamba uchafu ule ulikua ukimwagika nje kwenye jukwaa ambalo watu walikua wamekaa, na kusababisha usumbufu mkubwa wa waliokua wamekaa eneo/jukwaa lilipo karibu na chooni.

       Ushauri:
 • Wakati mwingine kukitokea tamasha kubwa kama hili ni vyema waandaaji wafanye utaratibu wa kuuza tiketi sehemu tofauti na pale getini na ikiwezekana waanze kuuza tiketi siku moja kabla ya tamasha au siku hiyo ya tamasha tiketi zianze kuuzwa asubui na mapema. Na kusiwe na utaratibu wa kuuzia tiketi mlangoni maana mara nyingi husababisha msongamano/foleni kubwa sana.
 • Ni vyema wakati mwingine mkatafuta watu wa uhakika wenye uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha makubwa ili kuweza kufahamu zaidi maana tunaamini unapokosea jambo ndio mwanzo wa kujifunza na pia kuongeza ufanisi zaidi.
 • Waliopata nafasi ya kuchoma nyama pia walishindwa kufahamu wakati gani ulikua wakati sahihi wa kuchoma nyama maana nyama ilikua ni ya kuunga foleni na wakati tamasha linamalizika wachoma nyama ndio kwanza wanaweka nyama na kuku kwenye jiko wakati watu ndio wanaondoka. Watu wengine waliondoka na njaa kwa kuwa nyama ilikua ya kusubiria muda mrefu.
     #teamKINGJOFA

No comments:

Post a Comment