Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 14, 2013

CHADEMA WASHINDA KATA ZOTE NNE KATIKA UCHAGUZI WA MADIWANI JIJINI ARUSHA ...!

Hawa ni baadhi ya wasimamizi wa kura za uchaguzi mdogo wa udiwani kata Temi jijini Arusha.
LEO tarehe 14 July 2013 ni siku ya kihistoria katika jiji la Arusha kwa kuwa ndio siku iliyokua ikisubiriwa na watu wengi ili kuona ni kitu gani kitakachojiri katika zoezi zima la uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne za jiji la Arusha. 
Na kwa mujibu wa repoters wa mtandao huu wa King Jofa Blog ni kwamba CHADEMA wameibuka kidedea kwa kuweza kushinda katika uchaguzi huo mdogo wa madiwani katika kata zote nne. Ambapo awali uchaguzi huo uliingia dosari baada ya shambulio la bomu lililorushwa katika uwanja wa soweto siku moja kabla ya uchaguzi na hatimae uchaguzi huo kuairishwa na kufanyika leo jumapili ya tarehe 14 July 2013.
Uchaguzi umefanyika ambapo leo umeonekana kuwa na utulivu mkubwa na hatimaye zoezi lakupiga kura na kuzihesabu kura limekamilika majira ya jioni. 
Endelea kutembelea www.kingjofa.blogspot.com kwa habari zaidi kuhusiana na uchaguzi huo wa madiwani.

No comments:

Post a Comment