Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 14, 2013

UPDATES: SHUHUDIA PICHA 9 ZA AJALI YA FUSO BAADA YA KUGONGANA NA BASI LA METRO COACH ILIYOTOKEA JANA USIKU.

 
Huu ni upande wa mbele wa fuso iliyopata hitilafu katika breki na kusababisha ajali.

 Hii ni fuso iliyokuja kuchukua (kufaulisha) mzigo uliokua kwenye fuso iliyopata ajali.

Baadhi ya watu wakiwa katika eneo la ajali wakifaulisha mzigo wa ndizi katika fuso nyingine. 

 Aliyesimama ni team leader wa #teamKINGJOFA akiwa anamujulia hali kondakta wa basi la Metro coach katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi.

 Kulia ni King jofa akiwa akipata katika eneo la ajali akipata maelezo kutoka kwa kondakta wa fuso aliyejitambulisha kwa jina la Remeni, muda mfupi baada ya kondakta huyo kuruhusiwa kutoka hospitali.

 Haya ni mabaki ya fuso iliyogongana na basi la Metro coach maeneo ya kawawa road nje kidogo ya mji wa Moshi.

 Haya ni mabaki ya ndizi yaliyotoka kwenye fuso iliyopata ajali.

 Huyu ni dereva wa fuso Godluck maarufu kama Mmasi akiwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi.

 Huu ni mkononi wa dereva wa fuso Mmasi akiwa na pingu kwa ajili ya taratibu za kiusalama.
 
 JANA usiku majira ya saa moja ajali mbaya na yakusikitisha iliyotokea eneo la barabara ya kawawa (kawawa road) iliyosababishwa na gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 615AWB inayomilikiwa na Dickson maarufu kama POPA D. Kugongana na basi la Metro Coach linalofanya safari za Dar - ArushaChanzo cha  ajali hiyo ni fuso iliyokua ikitokea maeneo ya kibosho ikiwa imebeba ndizi na maparachichi yaliyokua yakipelekwa Dar es salaam. 
Ambapo fuso hiyo ilipofika eneo lenye mteremko hatua chache kabla ya kufika kwenye eneo la ajali gafla dereva alijaribu kushika breki na kugundua kua gari haina breki ndipo alipoanza kujitetea kwa kujaribu kukwepa lori lililokua mbele yake ndio gari ikamshinda na kukutana uso kwa uso na basi la Metro Coach. Ajali hiyo iliyopelekea dereva wa basi la Metro Coach kupoteza maisha. Na baadhi ya majeruhi kuwahishwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Katika fuso kulikua na watu watatu ambao ni dereva wa fuso aliyejitambulisha kwa jina moja la Godluck maarufu kama Mmasi, Remeni ambaye ni kondakta na Mwenye mzigo ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka. Ambapo majeruhi wengine wamesharuhusiwa ila walipo hospitalini mpaka sasa ni dereva wa fuso (Godluck maarufu kama Mmasi), aliyekua amekodisha Fuso pamoja na kondakta wa Metro coach (Issa Dengu)

No comments:

Post a Comment