Juzi nikiwa mahakamani Tabora kulia kwangu ni M/Kiti wa Chadema Tabora Kamanda Mbaruk, kushoto ni shemeji yangu Kamanda Bella.
Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia MAHAKAMA KUU ambapo
nilishuhudia jaji akifanya kazi yake kwa busara iliyopitiliza (kwa maoni
ya Wakili msomi Peter Kibatala)
Kamanda wangu Mume wangu (kombati nyeusi) na shemeji zangu wakiingia mahakamani jana mjini Tabota.
Masuala ya Mahakamani yanaitaji subira ya hali ya juu hivyo bado
naendelea kumfariji Mpenzi wangu Kilewo ya kwamba mambo haya yatapita
tu. zaidi ya hapo namwombea sana.
Kushoto kwangu ni kamanda wa Chadema Tabora (huyu mama) na kulia ni mke mwenzangu (mumewe yupo kesi moja na mume wangu)
Kwa maoni ya Wakili Msomi PK ni kwamba Jaji alichukulia kesi hiyo kwa
uzito wake na pia akaheshimu na kuzingatia hali halisi ya Wakili, kwamba
anatoka mbali Dar es salaam na hivyo akaamuru Hoja za pande zote mbili
zipelekwe kimaandishi kuwaondolea usumbufu hasa wapeleka maombi ambao ni
sisi tunaosafiri kila siku. Na kwa sababu hizo basi tar 30july Jaji
atataja tar ya uamuzi.
No comments:
Post a Comment