Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, July 20, 2013

HUYU NDIO ASKARI WA TANZANIA ALIYEDAIWA KUTEKWA NA WAASI WA KUNDI LA M23 NCHINI CONGO...!

WAASI wa kundi la M23 wa DR Congo, wametoa taarifa kuwa wamemkamata askari wa Tanzania anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka 1994.
Waasi hao wa kundi la M23 wameweka picha ya passport ya askari huyo wa Tanzania kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. 
Kwa mujibu wa chimpreports.com, M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook ikiambatana na picha hiyo:
“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. 
Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”
christopher-george-yohana
 
Na hapa chini ndio M23 walichopost Twitter:




m23-tanzania-twitter 
 Hata hivyo uchunguzi wa awali uliofanyika kuhusu picha na pasport hiyo unaonyesha hakuna taarifa zozote za uhakika kuhusu swala hilo, huku ikielezwa kwamba pasporti hiyo iliyotangazwa na kikundi cha M23 huenda ikawa iliokotwa au walimteka raia wa Tanzania wakamuua na kuchukua hati yake ya kusafiria.

Baadti ya askari  wa JWTZ waliochunguza hati hiyo ya kusafiria wamedai kwamba, sheria za kazi hazimruhusu askari kutumia hati ya kusafiria akiwa amevaa mavazi ya kiraia hasa wanapokwenda kwenye operesheni zozote za kikazi.
 




No comments:

Post a Comment