MH. ZITTO KABWE ATOA UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA Tshs. 1000 KWA KILA SIMCARD KWA MWEZI...!
Mh. Zitto Kabwe
Finance Act, section 11 6(C) introduces #simcardtax
"(6C) There shall be charged an excise duty on telecommunication sim card at the rate of shillings 1,000/= per month."
Kifungu cha 11 kinaongeza kifungu cha 6C kwenye kifungu cha 124 cha Excise (Management and Tariff) Act CAP 147. Kwa kiswahili
"kutakuwepo na tozo la ushuru wa bidhaa (excise duty) la Tsh 1,000 kwa mwezi kwa kwa kila SimKadi"
Nini kilitokea? (What transpired)
Mwishoni mwa mwaka jana, 2012, Spika Anna Makinda aliunda Kamati ya
kufanya uchunguzi kuhusu vyanzo vya mapato ya Serikali. Kamati ili
iliongozwa na Mbunge wa Bariadi ndugu Andrew John Chenge. Moja ya
mapendekezo ya kamati ile ni kuanzishwa kwa kodi hii ya simkadi. Taarifa
ya kamati ile ilipelekwa Serikalini na haikuwahi kujadiliwa na Bunge
(licha ya rasilimali fedha ya Bunge kutumika kuendesha kamati ile).
Waziri wa Fedha, ndugu Mgimwa, alipokuwa anasoma Hotuba ya Bajeti mwezi
Juni mwaka 2013, alitamka kuwa kifungu cha kuanzishwa kodi hiyo hakipo
tena (ilikuwa tshs 1470 kwa mwezi). Kifungu hiki kilikuwa kwenye hotuba
yake. Inaonyesha kuwa huko Serikalini hawakuelewana kuhusu jambo hili na
hivyo kuamuriwa kufutwa (kulikuwa na Baraza la Mawaziri asubuhi ya siku
Bajeti inasomwa).
Hivyo pendekezo hili halikujadiliwa kabisa na
Bunge kwenye mjadala wa Bajeti ya Serikali na KWA HIYO halikupitishwa
kwenye Makadirio ya Mapato ya Serikali.
Baada ya Bajeti kupita,
Bungeni huletwa miswada 2, mmoja ni mswada wa matumizi (appropriation
bill) na mwingine ni muswada wa mapato (Finance bill). Katika muswada wa
Mapato hapakuwa na kifungu cha kutoza kodi hii ya simkadi.
Wizara
ilipoenda kwenye Kamati ya Bajeti, ili kupitia muswada huu, Kamati ya
Bajeti ikahoji ni kwa nini pendekezo lake limekataliwa na Serikali?
Hatimaye Kamati ya Bajeti ikashinda na kifungu cha kodi ya simkadi
kikaingizwa kwenye muswada wa Fedha 2013/14 kupitia jedwali na
marekebisho.
Baadhi ya wabunge kama John Mnyika waliandika jedwali
la marekebisho kupinga pendekezo hili lakini kwa kuwa majedwali yote
yalikuwa yakiishia kwenye kamati ya Bajeti ya Bunge, marekebisho yao
yakagonga mwamba.
Hatimaye Bunge lilipitisha Muswada huu na kuwa Sheria.
Nadhani kwa umuhimu wa historia ni vema kupata hansards za mjadala
mzima wa sheria ya Fedha mwaka 2013/14 ili kuweka kumbukumbu ya mbunge
gani alichangia nini na namna gani sheria ilipitishwa kifungu kwa
kifungu. Pia ni muhimu sana kujiuliza ni kwa nini baada ya sheria hii
kupita tarehe 29 Juni mwaka 2013, kulikuwa na ukimya mkubwa na hakuna
aliyepaza sauti mpaka wananchi walipoanza kuhoji kupitia mitandao ya
kijamii.
No comments:
Post a Comment