Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika Hitma ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni,Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally iliyosomwa katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika kuwaswalia Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,na Cpl Mohammed Juma Ally ,mbele katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo,wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,baada ya kuwasilim katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) na viongozi wengine walihudhuria katika mazishi ya Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udungo katika Kaburi la Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,aliyezikwa leo Mwanakwerekwe Mjini Unguja, akiwa ni miongoni mwa wanajeshi wa jeshi la Ulinzi la Tanzania 7 waliouwawa hivi karibuni Nchini Sudan Jimbo la Daafur
Baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally ,waliofurika katika viwanja vya makaburi ya Mwanakwerekwe,ambapo ndipo walipozikwa leo,mchana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Vingozi na Waislamu,wakiangalia Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania,walipokuwa wakitoa hesha ya mwisho kwa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
leo umeungana na viongozi mbali mbali wakiwemo wa vikosi vya ulizi na
usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar pamoja na wafiwa na wananchi katika mazishi ya
wanajeshi wa Zanzibar waliouwawa huko Darfur Jumaamosi ya Julai 13 mwaka
huu.
Majira
ya saa nne za asubuhi Dk. Shein akiwa pamoja na Makamu wa Kwanza wa
Rais Maalim Seif Sharif Hamad walishiriki katika duwa ya Hitma
iliyosomwa kwa ajili ya maiti zote mbili pamoja na kuwasalia maiti hao
huko katika masjid Noor Mohammad (S.A.W), Mombasa kwa Mchina, Mkoa wa
Mjini Magharibi Unguja.
Wananchi,
wafiwa pamoja na viongozi mbali mbali wa vyama na serikali walihudhuria
katika Hitma hiyo ambapo mapema Dk. Shein alitia saini vitabu vya
maombolezi kwa ajili ya marehemu hao huko katika eneo hilo la masjid
Noor Mohammad (S.A.W).
Baada
ya kumaliza dua na sala hiyo ya maiti Dk. Shein, aliongozana na
viongozi wengine na wananchi walielekea katika Makaburi ya Mwanakwerekwe
kwa ajili ya mazishi ya marehemu hao.
Katika
makaburi ya Mwanakwerekwe mamia ya wananchi walikuwa tayari
wameshajipanga kwa ajili ya kuwaaga narehemu hao ambao wote wamezikwa
katika eneo hilo maarufu la makaruni liliopo Wilaya ya Magharibi Mkoa wa
Mjini Magharibi Unguja.
Mbali
ya wananchi hao waliokuwa wameshafika na kujipanga katika eneo hilo la
makaburi nao wanajeshi wa kikosi cha Ulinzi cha JWTZ walikuwa
wameshajipanga vyema kwa ajili ya kuwaagaa wenzao kwa mila, desturi na
taratibu zote za Kijeshi kama ilivyo desturi.
Katika
eneo hilo la Makaburi la Mwanakwerekwe, Dk. Shein aliungana na viongozi
mbali mbali wa vyama na Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama vya SMT
na SMZ na wananchi pamoja na wafiwa.
Taratibu
za mazishi zilianza katika eneo hilo ambalo makaburi mawili yaliokuwa
yamechimbwa karibu karibu, mwili wa marehemu Sajenti Shaib Shehe Othman
ulianza kuzikwa kwa kuanza na taratibu zote za kijeshi na baadae kufuata taratibu za kuzika za kidini.
Mara baada ya kuzikwa kwa mwili wa Marehemu Sajenti
Shaib Shehe Othman, mwili wa marehemu Koplo Mohammed Juma Ali ulizikwa
pembezoni mwa kaburi hilo na kufuata taratibu zote za kijenshi na baadae
taratibu za kidini.
Baada
ya hatua hiyo ya mazishi salamu za Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Mrisho
Kikwete zilitolewa ambapo salamu hizo zilitoa pole kwa wafiwa na
wanafamilia wa marehemu na kuwaombea kwa MwenyeziMungu aziweke roho za
marehemu mahala pema peponi.
Aidha,
salamu hizo zilieleza kuwa msiba huo ni wa Taifa zima na si kwa upande
wa Tanzania pekee bali ni Afrika na dunia nzima kwa ujumla.
Nao
wanafamilia na wazazi wa marehemu hao, walitoa shukurani zao za dhati
kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kwa juhudi kubwa ilizozichukua katika kuhakikisha marehemu hao
wanafika katika maeneo yao ya kuzikwa kwa kufanikisha taratibu zote za
usafiri kwa ufanisi mkubwa.
No comments:
Post a Comment