Hawa ni baadhi ya vijana wa SOMJO DJ wakiwa kazini na hawa ni ambao wapo katika kikundi cha sarakasi.
SOMO DJ entertainment ya mjini
Moshi ilianzishwa mwaka 1996 na vijana wawili ambao ni Athumani Mganga maarufu kama Somjo na Ramadhani. Vijana hawa walikua na ndoto ya
kuhakikisha wakazi wa mji wa Moshi wanapata burudani na pia wanakua mfano mzuri
wa kuigwa na vijana wengine kwa kuamua kujiajiri wenyewe. SOMJO DJ wameendelea
kufanya vizuri sana
katika burudani na pia wameweza kuongeza ajira kwa vijana zaidi ya ishirini
ambao wamekua wakijipatia kipato kupitia kazi mbalimbali ambazo zimekua
zikisimamiwa na SOMJO Dj katika matamasha mbalimbali wamekua wakitoa nafasi kwa
vikundi vya sarakasi, dancers, Dj’s, presenters, na wengine wengi.
SOMJO DJ kwa sasa wanamiliki Vyombo
vya mziki (Sound System) vyenye dhamani ya zaidi ya milioni hamsini ikiwa ni
Generator tatu, Sound system kubwa mbili na Sound system ndogo moja, pia wana
Stage/Jukwaa moja kubwa lenye uwezo wa kugawanywa na kutoa majukwaa matatu. Na
pia SOMJO DJ wanaifurahia sana kazi yao na wanasema kazi hii ni nzuri kama mtu
atakua makini kuifanya ila ni kazi mbaya kama mtu atakua anaifanya bila kuwa
makini maana ni kazi ambayo inakuweka karibu sana na pombe na warembo, kwa
maana hiyo usipokua makini utajikuta maisha yako yanakosa muelekeo na kuishia
kwenye pombe na warembo.
GRARAMA ZA KUKODISHA
VYOMBO VYA MUZIKI
*Vyombo vya mziki (Sound System) bei ni kuanzia laki moja
(Tshs. 100,000) hadi milioni moja (Tshs. 1,000,000)
*Stage (Jukwaa) laki moja (Tshs. 100,000) hadi laki tano
(Tshs.500,000)
Kwa yeyote anayehitaji vyombo vya
mziki (Sound System) au Stage (Jukwaa) apige namba hizi 0715 882 373 au
0767 882 373.
Athumani Maganga almaarufu Somjo akiwa anaweka mitambo sana muda mchache kabla ya kazi kuanza.
MAFANIKIO YA SOMJO DJ
*Athumani Mganga ambaye ndie kiongozi na msimamizi wa SOJMO
DJ amefanikiwa kujenga nyumba kubwa (self container) yenye sebule, jiko, store
na vyumba vinne vya kulala (four bed rooms) chumba kimoja kikiwa ni master bed
room.
*Na pia ameshanunua kiwanja (plot) nyingine na tayari
amenunua vifaa vya ujenzi (materials) na wiki ijayo anatarajia kuanza shuhuli
za ujenzi wa nyumba ya pili.
*Na kwa sasa tayari anamiliki gari aina ya Toyota Hiace.
*Wamefanikiwa kukutana na kufahamiana na watu mbalimbali
kutokana na kazi wanazozifanya.
*Na baadhi ya mampuni ambayo SOMJO DJ wameshafanya nazo kazi
ni Serengeti Breweries, VodaCom, TBL, TiGo, Star Times, TPC, Redds, na mengine
mengi.
Hii ndio nyumba ya Athuman a.k.a Somjo aliyofanikiwa kuijenga kupitia kipitia kazi yake ya kukodisha vyombo vya muziki (Sound System)
CHANGAMOTO
*Changamoto wanazokutana nazo mara nyingi ni pale wanapopewa
kazi na mtu ambaye sio muhusika (dalali) wakati wa makubaliano wanakubaliana
vizuri lakini wanapoenda kwenye eneo la kazi wanakuta kazi ni tofauti na
walivyokubaliana. Na unakuta dalali amechukua hela nyingi kwa mteja alafu
anawalipa SOMJO DJ hela kidogo tofauti na ukubwa wa kazi yenyewe.
MATARAJIO YA SOMJO DJ
*Matarajio ya vijana hawa ni kuwa na vyombo vya muziki (Sound
System) na Jukwaa (Stage) ambavyo vyombo vyote hivyo wanatarajia viwe na dhamani
ya milioni mia moja au zaidi.
*Na pia wanatarajia kuanzisha mashindano ya u’DJ (DJ’s
competition) kwa mkoa wa Kilimanjaro ili kuweza kuwapata na kuwasaidia vijana
wenye uwezo wa kufanya kazi ya u’DJ.
MAFUNZO NA
AJIRA KWA VIJANA
*SOMJO DJ wanatoa mafunzo kwa kijana yeyote mwenye kuhitaji
kujifunza kazi ya kufunga vyombo vya muziki (Sound System), kuwa MC au
Presenter, kuwa DJ, na mafunzo hayo yanatolewa bureeeee….. ila kinachotakiwa na
kijana awe na akili timamu, awe anajitambua na pia awe makini katika
mafunzo/kazi.
Kwa kijana yeyote anaye hitaji apige namba hizi hapa 0715
882 373 au 0767 882 373.
siku zote hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi. Hapa ni Athuman akiandaa box la speaker ili aweza kulipiga rangi.
Hapa kazi imekamilika na speaker zipo tayari.
No comments:
Post a Comment