Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 22, 2013

MFANYA BIASHARA WA MOSHI ALIYE JIREKODI AKIMLAWITI MFANYAKAZI WA DUKANI AKAMATWA

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limemkamata mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, anayefahamika kwa jina Totolii Kimath anayetuhumiwa kwa kurekodi video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani anayefahamika kwa jina lmoja la Halima. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz, aliuambia mtandao huu kuwa kijana huyo ambaye anamiliki maduka matatu ya kurekodi na kuuza CD katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini Moshi, alikamatwa juzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA (Kilimanjaro Internationa Airport) akitokea Dubai alipokua amekimbilia baada ya sakata la video hiyo kuvuja. kamanda Robert Boaz alisema Jeshi la Polisi lilikuwa likifanya uchunguzi kwa muda mrefu wa picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na simu ambazo zinaonyesha mwanaume na mwanamke wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile. “Tulikuwa tunafanya uchunguzi wa picha zilizosambaa kwenye mitandao pamoja na simu kwenye Whatsapp ambazo zinaonyesha watu wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile, kimsingi ni kosa la jinai ambalo linatambulika kisheri katika kifungu namba 154 mwanamke kumruhusu mwanaume amuingilie kinyume cha maumbile ama mwanaume amuingilie kinyume na maumbile,” alisema. Alisema bado uchunguzi wa picha hizo unaendelea ikiwa ni pamoja na kumhoji mhusika na kwamba endapo uchunguzi utakamilika atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushiriki kufanya mapenzi kinyume cha maumbile. Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile. Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu ulibaini kuuzwa kwa video hizo ambazo zina vipande viwili, kimoja kikiwa na urefu wa dakika 8:47 na kingine dakika 4:00 kwa kiasi cha kati ya sh 3,000 hadi 10,000 katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi. Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo ambaye anamiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi Moshi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta ambazo moja kati ya vipande hivyo inaonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo wa kike. Katika hatua nyingine, taarifa mbalimbali kutoka eneo la stendi kuu ya mabasi zinasema baadhi ya wasichana wanaodaiwa kufanya mapenzi na kijana huyo wameingiwa na hofu kutokana na video nyingine ambazo zinadaiwa kurekodiwa na kijana huyo akifanya nao mapenzi. “Hapa stendi sasa hivi mabinti waliotembea na jamaa wako roho juu maana tayari wamepata habari kuwa mshikaji alikuwa akirekodi kila msichana aliyetembea naye, sasa wana hofu kuwa video zao pia zitasambaa kama zilivyokuwa hizi nyingine,” alisema kijana mmoja muuzaji wa duka la CD ambaye hakupenda jina lake kutajwa katika mtandao huu.


Credit: Dixon Busagaga

No comments:

Post a Comment