Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 7, 2013

MFANYABIASHARA WA MADINI YA TANZANITE ERASTO MSUYA AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI

 
Mwili wa Erasto Msuya ukiwa chini baada ya kupigwa risasi.
 
MFANYABIASHA maarufu wa madini aina ya Tanzanite ambeye pia ni mmiliki wa hotel ya kitali ya S.G Resort ya jijini Arusha anayefahamika kwa jina la Erasto Msuya amefariki dunia leo majira ya alasiri baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakati alipokuwa akitokea Mirerani akielekea jijini Arusha.

Taarifa kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo zinaeleza kuwa Bwana Erasto Msuya alisimamishwa na watu hao karibu na njia panda ya KIA (Kilimanjaro International Airport) na aliposimama walimtishia kwa kutumia bastola na kumtaka afate matakwa ya watu hao ndipo Erasto alipotoa bastola ili aweze kujitetea ndipo majambazi hao walipo amua kumpiga risia ambazo idadi yake haikuweza kufahamika kwa haraka.

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo endelea kutembelea   www.kingjofa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment