Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 15, 2013

TAZAMA PICHA 6 ZA AJALI ILIYOTOKEA JIONI HII

Hii ndio gari aina ya corrola 11 iliyogongwa na daladala.
Hawa ni baadhi ya mashuhuda wakiwa katika eneo la ajali.

Kulia ni askari wa barabari akiongea na sereva wa daladala pamoja na dereva wa corrola.

Huyu ndie Saidi Ally dereva wa daladala aliyesababisha ajali.
Picha ya juu ni Peter Swai dereva wa corrola iliyopata ajali.

Baada ya makubaliano kati ya madereva wote wawili sasa askari wa barabarani na dereva wa daladala iliyosababisha ajali wakiingia kwenye gari ili waelekee kituo cha polisi.

Leo jioni majira ya saa kumi na mbili kasoro imetokea ajali maeneo ya mnara wa saa uliopo Moshi mjini mita chache kufika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani. Ajali hiyo ilisababishwa na Daladala yenye namba za usajili T917 AEJ iliyokua imetokea maeneo ya kiboriloni ikielekea Moshi mjini. Daladala hiyo ilikuta gari aina ya Corola 11 imesimama eneo la mnara wa saa ikisubiri foleni ya magari ipungue ili iweze kuingia barabara kuu na kuendelea na safari.

Ndipo Daladala hiyo iliigonga kwa nyuma gari hiyo aina ya corolla 11 na kusababisha uharibifu. Baada ya ajali hiyo kutokea dakika chache baadae kulikua na foleni kubwa sana ya magari maana siku za hivi karibuni mji wa Moshi umeanza kuwa na foleni kubwa sana hasa nyakati za asubui na jioni. Lakini askari wa barabarani walipewa taarifa na kuweza kuja katika eneo ilipotokea ajali hiyo.

Chanzo cha ajali hiyo kinasemekana ni uzembe wa dereva wa daladala kuendesha gari bila tahadhari na pia kutokufahamu sheria za barabarani. Baada ya ajali hiyo kutokea askari wa barabarini walifika katika eneo la ajali na kufanikiwa kupima na kuweza kuruhusu magari mengine kuendelea na safari maana baada ya kutokea kwa ajali hiyo barabara haikuweza kupitika kwa kuwa gari zilizopata ajali ziliziba barabara. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliye jeruhiwa ila gari zote mbili ziliumia..

Askari wa barabarani (traffic) walipofika eneo la tukio na kupima ajali na kugundua mwenye makosa, mmoja wa askari hao wa barabarani aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel (Emma) alitumia busara kubwa sana kuwashauri madereva wakubaliane ni jinsi gani dereva aliyesababisha ajali ataweza kulipa uharibifu aliousababisha katika ajali ile baada ya kukubaliana waende kituo cha polisi kutoa maelezo na kuandikishiana jinsi watakavyolipana. Pia askari huyo aliwaelimisha kuhusu sheria za makosa ya barabarani na mwisho dereva wa daladala akakubali kumlipa dereva wa corolla. 

No comments:

Post a Comment