Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 15, 2013

POLISI WAFANIKIWA KUMPATA MTU ANAYETUHUMIWA KUHUSIKA NA KIFO CHA BILIONEA ERASTO MSUYA.

 Aliyevaa miwani ni marehemu Erasto Msuya enzi za uhai wake.

Polisi  wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite  huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua  bilionea Erasto Msuya (pichani). Habari  za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara  huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na  makachero.
Kwa  mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za  kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa  fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.

“Tumewakamata  watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha  za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani  kwake,” alidokeza polisi mmoja.
Habari hizo  zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao  walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na  kutumika kupanga mauaji hayo.
Pikipiki  hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa nyumbani  kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji  na zote zimekamatwa.
Mahojiano  kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na  katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri. lakini hakitatajwa jina lake.

Chanzo - Mwananchi

No comments:

Post a Comment