Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 18, 2013

HAYA NDIO YALIOJIRI MAHAKAMANI KATIKA KESI YA MAUAJI YA MFANYA BIASHARA WA MADINI ERASTO MSUYA

 Mtuhumiwa namba moja, Sharifu ‘Athumani’ Mohammed (31), wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Erasto Msuya, akiwasili mahakamani, katika Mahakama ya hakimu mkazi 
Moshi, Kilimanjaro.mtuhumiwa huyo na wenzake 6  anatuhumiwa kumuua msuya mnamo tarehe 7 August 2013 kwa kumpiga risasi.

 Maelfu ya wananchi waliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wakifuatilia kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini aina ya Tanzanite, katika mji mdogo wa Mererani, Erasto msuya, aliyeuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. 

 Maelfu ya wananchi waliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wakifuatilia kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini wa Mererani, Erasto msuya , aliyeuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. 

Baadhi ya ndugu wa marehemu, Erasto Msuya awaliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wakimpakiza Mama yao (jina halikufahamika maramoja) kumkimbiza katika Hospitali ya KCMC baada ya kuanguka na kupoteza fahamu mahakamani hapo.

HABARI KAMILI::

KESI ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Erasto Msuya (43), imelazimika kusikilizwa katika mahakama ya ndani baada ya kutokea sintofahamu huku mmoja wa waandishi wa habari aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo akishambuliwa na ndugu wa Marehemu.
Kesi hiyo iliyotajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu Mkazi Moshi, Agosti 21 mwaka huu, ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya wazi lakini kutokana na kuwepo kwa umati mkubwa mahakamani, kesi hiyo ilihamishiwa mahakama ya ndani jambo lilowakera ndugu wa marehemu.
 Baada ya kuambiwa kesi hiyo imehamishiwa mahakama ya ndani, Ndugu wa Marehemu walionesha kukerwa na kitendo hicho na kuanza kufanya vurugu na kulazimisha maaskari wa mahakama kuingilia kati wakisaidiwa na wale wa kutuliza ghasia (FFU).
Katika tukio hilo, waandishi wa habari wachache walioruhusiwa kuingia kusikiliza kesi hiyo walijikuta katika wakati mgumu, huku mmoja wao, Venance Maleli wa kituo cha Redio cha Moshi FM akishambuliwa na wanandugu hao ambao pia walitishia kumnyang’anya kamera yake.
Tukio hilo halikuishia hapo kwani, Mwandishi wetu, alifanyiwa fujo na ndugu wa Marehemu ambao hawakutaka kupigwa picha wakati wakifanya juhudi za kumkimbiza hospitalini Mama yao, aliyepoteza fahamu baada ya kupata taarifa za kuahirishwa kwa kesi hiyo.
Aidha baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa mahakamani hapo walilazimika kuondoka kwa kujificha kwa kuhofia usalama wao.
Katika kesi hiyo dakika hiyo iliyochukua takribani dakika 25 tu, watuhumiwa wengine wanne waliunganishwa katika shtaka hilo la mauaji kwa kukusudia kinyume na kanuni namba 16, kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai.
Watuhumiwa hao ni Joseph Damas maarufu Chusa mkazi wa Jijini Arusha, Jalila Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, lakini pia anakaa Manyara na Kondoa , Sadiki Mohammed Jabir “msudani” au  “mnubi”(32), mkazi wa Dar es salaam na Langata wilayani Hai na Karim kihundwa (33) mkazi wa kijiji cha Lawate wilayani Siha na kufanya jumla ya watuhumiwa kufikia 7 mpaka sasa.

Hata hivyo maelfu ya wananchi waliofurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo, walionesha kukerwa na kitendo cha kutoruhusiwa kusikiliza kesi hiyo ambapo mara tu baada ya kesi hiyo kuahirishwa walionekana kukimbilia mlango wa kutokea.
Watuhumiwa hao wote 7 waliondolewa mahakamani hapo kwa ulinzi mkali wa Jeshi la polisi wakiwa wamepakizwa katika Gari ya polisi, namba za usajili T 743 ADC iliyokuwa na Madirisha Meusi (tinted).
Kesi hiyo inayoendeshwa na wakili wa Serikali, Stella Majaliwa akisaidiwa na Janeth Sikule katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Ruth Mkisi imeahirishwa hadi October 2 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.


Mwandishi: Immacheche wa #teamKINGJOFA
Mpiga Picha: Fadhili Athumani

No comments:

Post a Comment