Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 28, 2013

SHUHUDIA MAELFU YA WATU WALIOHUDHURIA KATIKA MAZISHI YA JAMES KOMBE MKOANI KILIMANJARO

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, kanda ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao akiendesha Ibada ya Maziko ya  aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyefariki dunia Oktoba 21 mwaka huu, Jijini Dar es salaam na Kuzikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akitoa heshima za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga (wakwanza) na Mkuu waWilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahimu Msengi (wa pili) wakitoa heshima zao za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi mkoanbi Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz akitoa Salamu za Rambirambi kwa niaba IGP Said Mwema katika ibada ya Maziko ya aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mheshimiwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Aisha Nyerere, akitoa heshima za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mke wa Marehemu, Maria Kombe (katikati) pamoja na watoto wake wakifuatilia ibada ya Maziko ya Mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati),  Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz (kulia) na Kaimu kamanda wapolisi mkoani Kilimanjaro, Moita Koka, wakitoa heshima za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, ukiondolewa kanisani katika kanisa la KKKT, usharika wa Msae kuelekea Nyumbani kwake kwa ajili ya zoezi ya Maziko yaliyofanyika Jana, kijijini Msae, kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.
Askofu Mkuu wa KKKT kanda ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao, akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi kilimanjaro, Robert Boaz na Kamanda wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas (mwenye suti) wakiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mke wa Marehemu, Maria Kombe, akiweka Ua katika Kaburi la Marehemu mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Wanafamilia wakiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Watoto wa Marehemu Kombe, wakiongozwa na Kaka yao, Dustan Kombe kuweka  Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.

Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Aisha Nyerere, akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Vijana wa Jeshi la Polisi, wakitoa Heshima za mwisho katika kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, kwa Mujibu waTaratibu zaKijeshi. Kombe alizikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. picha zote na Taifa Letu.com blog

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, amewaongoza Maelfu ya  waombolezaji katika mazishi ya Aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama  Barabarani, Kamishna mstaafu, James Kombe (63), aliyefariki dunia  October 21 mwaka huu katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es  salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kombe aliyeitumikia Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 24, katika  nyadhifa mbalimbali, alizikwa jana saa 9:40, alasiri, Nyumbani kwake  katika kijiji cha Msae, kata ya Mwika, Jimbo la Vunjo, wilaya ya Moshi  vijijini, mkoani Kilimanjaro baada ya ibada ya maziko iliyofanyika  katika Usharika wa Msae-Lyakrima na kuongozwa na Askofu Mkuu wa KKKT,
dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Martin F. Shao.

Akitoa Salamu za Rambirambi, Gama alisema serikali imeguswa na msiba  huo huku akimuelezea Marehemu Kombe kama mtu muadilifu, mwaminifu na  mtu asiyekuwa, asiyekuwa na ubinafsi na mzalendo aliyeitumikia Taifa  lake kwa nguvu zake zote hadi dakika za mwisho za uhai wake.

“Ni kweli mazingira yetu kikazi yanatofautiana, lakini ni wazi kuwa  kuna mengi ya kujifunza na kujivunia kutoka kwa Kamishna Kombe enzi za  uhai wake, Marehemu ameacha historia iliyotukuka nyuma yake, alikuwa  ni mtu mwadilifu sana, mwaminifu, mzalendo na mchapa kazi  aliyejitoleakulitumikia Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla,” alisema
Gama.

Kuhusu swala la uwajibikaji na utendaji kazi, Gama alisema wananchi  wengi kwa sasa wanashindwa kufanya kazi za maendeleo hasa mkoani  Kilimanjaro katika maeneo ya Rombo, Marangu na Mwika kutokana na  kukithiri kwa vitendo vya Unywaji pombe holela ambapo aliagiza wakuu  wa wilaya kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti hali hiyo.

Awali akiongoza Ibada ya Maziko, Askofu MKuu wa KKKT, dayosisi ya  Kaskazini, Dkt.  Martin Shao, aliwataka waumini wa dini ya Kikristo, wananchi pamoja na  watumishi katika Jeshi la Polisi kufanya yale yaliomema ikiwa kweli
wanataka kuenziwa kama ilivyo kwa Marehemu Kombe.

Dkt. Shao katika ibada hiyo alimuelezea Marehemu Kombe kama mtu  anayestahili kuenziwa daima kama anavyoenziwa Hayati Baba wa Taifa,  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka na utendaji wake kazi  uliotukuka, uzalendo na Uadilifu pamoja na uwajibikaji katika  kuhakikisha Amani ya Tanzania na usalama wa Wananchi wake.

Kabla ya kifo chake, Kamishna Kombe, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa  wa Kansa ambao ulianza kumsumbua Juni mwaka jana na kutibiwakatika  Hospitali ya Rufaa KCMC mjini Moshi.

James Kombe, aliyezaliwa mwaka 1950, mwika Kilimanjaro ameacha mjane mmoja, Maria Kombe na watoto watano na kwamba alilitumikia Jeshi la polisi kuanzia Machi, mwaka 1970 na kulitumikia mpaka alipostaafu mwaka 2010.

Akisoma historia ya Marehemu, Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani, Joseph Mwakabonga alisema Kamishna Kombe, alijiunga na Mafunzo ya awali machi 23 mwaka 70 na kumaliza Agosti 28 mwaka huo, huko Mopshi baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda.

Alisema alipandishwa vyeo kama Mkaguzi wa polisi (1977), Kamishna msaidizi (1995), Mkaguzi wa polisi (1986), mrakibu mwandamizi (1991) na Kamishna Msaidizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu 2010.




No comments:

Post a Comment