Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 26, 2013

MEYA WA MANISPAA YA MOSHI ASIKITISHWA NA MAAMUZI YA BARAZA LA HALMASHAURI

MOSHI meya wa manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Jaffari Michael, ameelezea kusikitishwa kwake na tabia ya maamuzi yanayopitishwa na halmashuari hiyo kutokutekelezwa na wahusishwa.

Michael alielezea kusikitishwa kwake huo wakati wa baraza la halmashuari hiyo lililokaa ambapo ilibidi kubadilishwa kuwa kamati, baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kutaka iwe hivyo ili kuwawajibisha watendaji wababaishaji katika kutekeleza maamuzi ya baraza la madiwani.

Alisema jambo hilo linazidi kuweka mashaka dhidi ya watendaji mbalimbali wa halmashauri hiyo ya kuwa wamebobea katika rushwa na kwamba katika siku za hivi karibuni, maeneo ya wazi yamekuwa yakilengwa na watendaji ambao si waaminifu kwa kuwagawia watu kwa misingi ya rushwa.

Akichangia hoja hiyo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaban  Ntarambe, alitoa rai kwa madiwani kuachana na wazo la kuligeuza baraza hilo kuwa kamati maalum kwa madai kuwa si rahisi kuigeuzwa kuwa hiyvo.

Pamoja rai hiyo, madiwani hao waliisimamia hoja yao ya kuligeuza baraza hilo kuwa kamati maalum baada ya meya Michael kuagiza kura zipigwe.

Madiwani hao walifikia uamuzi huo kufuatia malalamiko yaliyojitokeza kufuatia mtu mmoja kujenga eneo la wazi pamoja na halmashuari hiyo kuagiza litumiwe kujenga ofisi ya kata.

Madiwani hao walidai kuwa mara baada ya kuona kuwa eneo hilo limevamiwa na kuwekwa vifaa vya ujenzi ikiwemo mchanga, walitoa maamuzi ya kutaka vitu hivyo viondolewe bila mafanikio na badala yake ujenzi wa eneo hilo ulionekana kuendelea kujengwa ambapo pamoja na maamuzi kutolewa pabomolewe amri hiyo bado haijatekelezwa.

No comments:

Post a Comment