Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 30, 2013

SOMA HII NA UFAHAMU JINSI YA KUJIHADHARI NA UTAPELI WA HATARI ULIOIBUKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI

Hii ndio barabara ya rengue inayotokea mnara wa saa kuelekea TANESCO mpaka TRA ambapo utapeli huo hufanyika.

MOSHI Siku za hivi karibuni umeibuka utapeli wa kimazingira ambapo umekuwa tishio sana kwa wakazi wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.  Kumekuwa na tabia za baadhi ya watu ambao mpaka sasa majina yao hayajafahamika ila wamekuwa wakionekana sana maeneo ya  barabara ya rengua mjini Moshi karibu na zilipo ofisi za Tanzania Revenue Authority (TRA) mjini Moshi,  National Microfinance Bank (NMB) na Ofisi kuu za shirika la umeme Tanzania TANESCO.

Watu hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watano wanapotaka kumtapeli mtu ni kwamba mmoja wao humsogelea mtu huyo wanayetaka kumtapeli na kumsalimia na kujifanya yeye ni mgeni na anaulizia sehemu fulani baada ya kuuliza sehemu hiyo wakati huo wale wenzake huwa maeneo ya karibu. Unapomaliza kumuelekeza tapeli huyo sehemu aliyokuuliza anachokifanya ni kukushukuru kwa kukushika mkono na wewe bila hiana unapompa mkono akikuachia kama ni mwanamke utafungua pochi yako mwenyewe na kumtolea hela na kama ni mwanaume utaingiza mkono mfukoni na kutoa pesa na kumkabidhi. 

Baaada ya hapo matapeli wale hukodisha tax au pikipiki maarufu kama bodaboda na kutokomea pasipojulikana na kumuacha aliyetapeliwa akiwa kama vile amepigwa na butwaa na baada ya dakika chache akili za mtu aliyetapeliwa hurudi sawa na kutambua kuwa ameshatapeliwa pesa zake. Baada tukio hilo kufanyika kinachofuata ni mtu yule aliyetapeliwa kuanza kusikitika au wengine hupiga mayowe ya kuhitaji msaada kutoka kwa wasamaria wema kitu ambacho huwa ni kigumu sana kupata msaada maana matapeli wale wanakuwa wamesha tokomea pasipo julikana.

Na siku za hivi karibuni mama mmoja alikumbwa na utapeli huo ambapo yeye alitoka kuchukua kiasi cha shilingi milioni tatu pale National Microfinance Bank (NMB),  na anasema yeye alikutwa na utapeli huo baada ya kufatwa na kijana/tapeli mmoja aliyejifanya mgeni na kumuomba amuoneshe zilipo ofisi za mabasi ya Dar Express na mama alimuelekeza kijana yule baada ya hapo yule kijana/tapeli alimshukuru yule mama na kumpa mkono wa ahsante na hapo yule mama alifungua pochi na kutoa kiasi cha shilingi milioni tatu na kumkabidhi kijana/tapeli yule.  Baada ya hapo kijana yule aliita tax na kutokomea pasipojulikana. 

Kwa mujibu wa watu waliopo  maeneo unapofanyikia utapeli huo  wanasema  matapeli hao huonekana sana tarehe za mwisho w mwezi ambapo wanajua kuwa watu wengi huenda kuchukua pesa zao pale National Microfinance Bank (NMB), na wengine huwa wanaenda kuchukua maelezo pale Tanzania Revenue Authority (TRA) kwa ajili ya kwenda kulipa kodi mbalimbali za serikali.

No comments:

Post a Comment