Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 31, 2013

MWANAUME MMOJA AMEWAFANYIA UKATILIA WATOTO WAWILI WENYE UMRI USIOZIDI MIAKA 13.

MOSHI Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Kiria kata ya Mamba kusini, wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, amewabaka na kuwaingilia kinyume cha maumbile watoto wake wawili wenye umri wa miaka 10 na 13 na kuwajeruhi vibaya.

Kitendo cha baba huyo kufanya mapenzi na watoto wake, kiliwagusa wanawake wa kijiji hicho ambao waliungana na kumkamata mwanaume huyo bila kuhitaji msaada wa wanaume na kumpeleka kituo cha polisi kilichopo Himo huku wakitishia kumuua kutokana na kitendo cha polisi kumwachia huru, kila anapofikishwa polisi kuhusiana na unyama anaowafanyia watoto hao.
 
Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji cha Kiria Doroth Mtui amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani wa watoto hao alilazimika kufika nyumbani kwa mtuhumiwa kuzungumza na mtoto huyo ambae alimweleza ukatili anaofanyiwa na baba yake na ndipo alipopiga “ yowe” kuita wananchi wengine ambao waliandamana kwa pamoja na kumkamata mwanaume huyo na kumpeleka kituo cha polisi Himo.

Amesema baada ya kufika kituo cha polisi Himo, walimpeka mtoto huyo hospitalini, ili kuthibitisha kama kweli amebakwa ambapo taarifa iliyotolewa na daktari wa hospitali teule ya Kilema, ilionyesha kuwa mtoto huyo ameingiliwa sehemu zote mbili na kwamba ni kitendo ambacho kilianza muda mrefu na kusababisha kuota nyama sehemu zake za siri.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Roabart Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi tayari wamefanya uchunguzi na kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote.

No comments:

Post a Comment