Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, October 6, 2013

TAZAMA PICHA 17 ZA YALIYOJIRI KWENYE SERENGETI FIESTA 2013 MKOANI KILIMANJARO




Huyu anaitwa Hyper Kid mshindi wa Super nyota atakaye uwakilisha mkoa wa Kilimanjaro jijini Dar es salaam.

Ney Lee ndio msanii wa kwanza kulifungua jukwaa la Serengeti Fiesta Moshi 2013 kati ya wasanii waliokuwa kwenye ziara ya Fiesta Kilimanjaro. 
Ndege mnana Linah Sanga akitoa burudani kwa mashabiki wake waliohudhuria katika Serengeti fiesta 2013

Mshindi wa BSS mwaka jana Walter Chilambo aiwa jukwaani.

Ally Nipishe akisalimiana na mashabi wake. 

Real man Ney wa Mitego awapa mashabiki salamu zao.
Dj Fetty wa Clouds FM nae alikuwa akifanya yake.

Jambo Squard a.k.a mamong'o wakiudhihirishia umati wote kuwa wao ndio majogoo vichaa.

Dully Sykes akiwafundisha mashabiki wake wa moshi Bongo flavour.

Kundi la Weusi Joh Makini, Niki wa Pili na G Warawara wakiwakifanya Hip Pop buttle kwenye stage
.
Mtu mzima J. Martin akisema na mashabiki wake.

J. Martin na Mwana FA.

Mwana FA, AY na J. Mrtin wakipagawisha.

 
Kutoka Kushoto ni Babi, DJ Virus na DJ Drill. 

 
Upendo (Mama Johnson) kushoto akiwa na Manueltok.
Hizi ni shangwe za Serengeti Fiesta 2013 Moshi - Kilimanjaro
Haqa ni baadhi ya mashabiki waliohudhuria katika Serengeti fiesta 2013 uwanja wa Majengo mjini Moshi.

 Hii ndio hali ilivyokuwa kwenye uwanja wa majengo.

       Serengeti Fiesta 2013 iliyofanyika katika uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro iliweza kutoa ajira tofauti  tofauti za muda (temporary work)  kwa wakazi  wa mkoani Kilimanjaro zaidi ya hamsini,   ajira hizo ni kama vile kufanya matangazo ya barabarani, ulinzi wa kwenye milango ya kuingia ndani ya uwanja wa majengo, ulinzi wa ndani kwa raia na mali zao, kuuza vunywaji kwa wateja/raia waliokuja kufurahia fiesta, wasaidizi wa kufunga jukwaa, kizalisha umeme (generator) na nyingine nyingi.
Pia ni tamasha kubwa ambalo limeweza kuwapa watu nafasi ya kupata burudani ya aina yake na pia kushuhudia kijana mmoja wa mjini Moshi anayefahamika kwa jina la Hyper Kid kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro kilichofanyika cha kumsaka msanii wa muziki wa kizazi kipya mkoani Kilimanjaro ambaye ataenda kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro kwenye Supper nyota jijini Dar  es salaam.
Uwanja wa majengo ni uwanja ambao hauna vyoo lakini waandaji wa fiesta waliweza kuweka vyoo vya muda na kwa kweli lilikuwa ni jambo jema sana na lililowafurahisha wengi . Kulikuwa na watu wengi sana lakini waandaji walikuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha kila raia anapata burudani, vinywaji, chakula na kuondoka akiwa salama yeye na mali zake.  
 Jambo lililowasikitisha wengi ni vitendo vya baadhi ya watu waliokuwa wamepewa jukumu la kulinda raia na mali zao kubadilika na kutumia nguvu nyingi kupita kiasi kutuliza vurugu. Hali hiyo ilipelekea baadhi ya watu kuona kama watu wa usalama hawawatendei haki raia lakini baada ya raia kuchachamaa waandaaji wa fiesta waliongea na watu wa usalama na hali ikawa shwari.

#teamKINGJOFA


No comments:

Post a Comment