Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 2, 2013

MASIKITIKO MAKUBWA: AANGUKA MTONI NA BAISKELI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO

Hao ni baadhi ya wanakijiji wa giza ulole wakimuweka sawa marehemu Alphonce ili wampakize kwenye gari kwa ajili ya kumpeleka kituo cha polisi kupata kibali cha kuupeleka mwili wa marehemu Alphonce kuuhifadhi katika hospital ya wilaya ya Hai.

Mwili wa marehemu Alphonce ukiwa kwenye gari tayari kwa kupelekwa katika kituo cha polisi cha Bomang'ombe na baadae kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Hai.

MOSHI jana jioni majira ya saa kumi na moja lilitokea tukio la ajabu katika mto Sanya eneo linalofahamika kama mamba nane kijiji cha Gizaulole katika mji mdogo wa Boma Ng'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. Sababu ya eneo hilo la mto huo kuitwa mamba nane ni kwasababu miaka ya nyuma ilisemekana eneo hilo lilikuwa na mamba wapatao nane na walikuwa ni tishio sana kwa wakazi wa kijijini hapo.

Lakini kwa sasa inasemekana mamba hao wametoweka lakini kuna chunusi ambao wamekua wakihatarisha sana maisha ya wanakijiji wa Gizaulole. Na mwanzoni mwa mwaka huu kuna kijana mdogo ambaye alikuwa akiogelea katika eneo hilo la mto na kuzidiwa nguvu na maji na kupoteza maisha. Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina Alphonce Mwiche mkazi wa Gizaulole jana jioni majira ya saa kumi na moja alitoka nyumbani kwake na kuelekea katika mto Sanya kwenda kutega samaki aina ya kambale, na inasemekana amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu. Lakini jana ilikuwa ni siku mbaya kwake na kwa wana kijiji wa Gizaulole.

Shuhuda wa tukio hilo aliyefahamika kwa jina moja la Mwalimu aliueleza mtandao huu wa www.kingjofa.blogspot.com kuwa alimuona Alphonce akiendesha baiskeli pembezoni mwa mto huo lakini baada ya dakika chache alisikia kishindo kikubwa ambacho kiliashiria kama kitu kizito kimedondoka ndani ya maji. Shuhuda huyo alikimbilia katika eneo hilo la mto na kutazama ndani ya maji ambapo anasema aliona mikono ya Alphonce ikiwa juu ya maji ikiashiria kuhitaji msaada. Shuhuda huyo alikimbia huku akipiga yowe za kuita watu waliokuwa karibu na eneo lile la mto kuja kutoa msaada. Watu wengi sana walifika eneo lile na baadhi ya vijana kuingia ndani ya maji kuanza kumtafuta Alphonce zoezi la kumtafuta kijana huyo lilifanyika kwa zaidi ya lisaa limoja lakini hatimae walifanikiwa kumpata akiwa tayari ameshafariki dunia. Kwa kila mwanakijiji aliyekuwa katika eneo lile alikuwa akimuelezea marehemu Alphonce kwa jinsi alivyokuwa mchapa kazi hodari.

Alikuwa akifanya kazi za aina mbalimbali kijijini hapo ikiwa ni pamoja na kulima, kujenga nyumba, kutengeneza bustani za mauwa na pia kutengeneza miti ya uzio wa nyumba. Hakika ilikuwa ni siku ya majonzi na simanzi kubwa sana kwa wanakijiji wa Gizaulole kwa kuondokewa na kijana kama yule aliyekuwa mfano mzuri wa kuigwa na vijana wengine.

Yeye mbele sisi nyuma yake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Mungu lihimidiwe.

#teamKINGJOFA






No comments:

Post a Comment