Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 26, 2013

WAZAZI WA WILAYA YA MWANGA WATAKIWA KUJIJENGEA TABIA YA KUHUDHURIA KATIKA VIKAO VYA SHULE

WAKAZI wa wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujijengea tabia ya kuhudhuria vikao vya kujadili maendeleo ya shule ili kuweza kufahamu maendeleo na tabia za watoto wao kuliko kuwaachia walimu majukumu hayo ya kuwaangalia watoto.

Swala hilo limetolewa na mkuu wa shule ya sekondari ya Maghare, Gerald Semindu, katika mahafali ya Tano ya kidato cha nne ambapo wanafunzi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya tisini wamehitimu masomo yao ya kidato cha nne katika shule ya sekondari
Maghare iliyopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Mkuu huyo wa shule Mr. Gerald Semindu amesema shule hiyo inakabiliwa na tatizo mbalimbali likiwemo la baadhi ya wazazi kutokupenda kuhudhuria katika vikao vya shule, na badala yake jukumu hilo wamewaachia walimu peke yao jambo ambalo linawawia vigumu sana. Maana mtoto anahitaji uangalizi wa wazazi na waalimu.

Mkuu huyo wa shuele a
mesema endapo wazazi watatimiza wajibu wao ipasavyo itasaidia kuweza kutambua tabia ya mtoto wake mapema awapo shuleni, na kumfanya mwanafunzi huyo kuwa na nidhamu na maendeleo kwa nyumbani na shuleni pia.
 
baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo, ni wazazi
kutolipa ada kwa wakati pamoja na michango mingine ya shule kwa wakati
hali ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi za taaluma katika
ufundishaji.

Akiendelea kuelezea changamoto nyingine za shule hiyo ni ukiosefu wa jengo la maabara ambalo ni muhimu sana kwa wanafunzi ambao wanasoma masomo ya sayansi, hali inayowafanya kushindwa kujifunza kwa vitendo, ukosefu wa bwalo na shule kutokuwa na umeme.

Mkuu wa wilaya ya Mwanga Shaibu Ndemanga, aliwataka
wananchi kutozibeza shule za kata na badala yake kuweka mshikamano kwa ajili ya kuziboresha shule hizo za kata ili watoto waendelee kupata elimu iliyo bora.

Amesema  katika shule ambazo zimekuwa mkombozi mkubwa kwa mwananchi wa kipato cha chini ni kuwepo kwa shule za kata, ambapo serikali itaendelea kuziboresha zaidi kwa kuwapatia walimu, vitabu pamoja na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

No comments:

Post a Comment