Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 22, 2013

WAFUNGIWA NDANI KWAMIAKA 30....,

Wanawake watatu wameokolewa baada ya kufungiwa ndani ya nyumba kama watumwa kwa miaka 30 katika mazingira mabaya nchini Uingereza.
Shirika moja la misaada lililowapa makao wanawake hao, limesema kuwa lilipigiwa simu na mwanamke mmoja aliyesema kua yeye pamoja na wenzake wawili walikuwa wanazuiliwa katika eneo moja Kusini mwa London.


 Aneeta Prem, kutoka shirika lililowaokoa wanawake hao nchini Uingereza Mwanamke mmoja raia wa Malaysia mwenye umri wa miaka 69, mwingine kutoka Ireland akiwa na umri wa miaka 57, na Muingereza mmoja mwenye umri wa miaka 30, waliokolewa tarehe 25 mwezi Oktoba. Lakini taarifa hii imejitokeza tu siku ya Alhamisi.

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 67 pamoja na mkewe, walikamatwa kama washukiwa katika mtaa wa Lambeth na kisha kuachiliwa hadi mwezi Januari kesi itakaposikilizwa.
Inspekta mmoja kwa jina Kevin Hyland, kutoka katika kitengo cha polisi cha kukabiliana na biashara haramu ya binadamu, alinukuliwa akisema," hii ndio awamu ya kwanza ya uchunguzi huu. Wanawake hawa wameathirika sana kimawazo, baada ya kuzuiliwa kwa miaka 30 katika mazingira mabaya bila ya kutoka nje na kujaribu kujua kilichofanyika katika kipindi cha miaka 30 , bila shaka itachukua muda mrefu.''
Wanawake hao walipatikana baada ya mmoja wao kuwasiliana kisiri kwa simu na shirika hilo la misaada
Wanawake hao hata hivyo walifanikiwa kutoroka wakati wenyeji wao walipokuwa wametoroka.
Haijulikani ikiwa wanawake hao wana uhusiano.
Maafisa walisema kuwa watu waliokuwa wamewazulia wanawake hao hawakuwa raia wa Uingereza na kua hawana uhusianao na mateka wao kwa sababu ya uraia wao.

No comments:

Post a Comment