Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 22, 2013

Mwathiriwa wa ubakaji akamatwa Somalia

Msichana mmoja amekamatwa mjini Mogadishu Somalia, baada ya kusimulia kituo kimoja cha redio nchini humo kuhusu alivyobakwa na watu waliomtishia kwa bunduki.
Mwandishi aliyemhoji msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 pia amezuiliwa.






Umoja wa Mataifa unataka uchunguzi ufanywe kuhusu madai hayo ukiwema kuwa unapiga darubini uhuru wa vyommbo vya habari na ambavyo serikali itachunguza kisa hiki.

Serikali ya Somalia inasema kuwa lazima haki itendeke.
Mapema mwaka huu , mwathiriwa mmoja wa ubakaji pamoja na mwandishi wa habari walifungwa jela mwaka mmoja ingawa waliachiliwa baadaye kutokana na uamuzi wa kesi ya rufaa.
Ubakaji na waandishi wa habari wanaoripoti visa vya ubakaji au dhuluma nyinginezo za kingono, ni mada ambayo huhofiwa kuzungumziwa nchini Somalia na kesi hii ndio ya hivi karubui kuhusu polisi kumkamata mwathiri wa ubakaji pamoja na mwandishi habari aliyemhoji.
Msichana huyo aliambia kituo cha redio cha Shabelle, kuwa alibakwa na waandishi habari wenzake wawili wakiwa akiwa ameshikiliwa bunduki.
"mmoja alinitishia kwa bunduki na kunipeleka chumbani kwa nguvu , na kunivamia huku akinivunjia heshima yangu, '' msichana huyo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema katika video kwenye mtandao wa Redio Shabelle.
"ninaomba serikali kuchukua hatua dhidi ya wabakaji hawa, huenda wamewatendea unyama huu wasichana wengine wasio na uwezo wa kujitetea,'' alisema msichana huyo.
Video hiyo imepeperushwa kwenye mitandao mingine ya habari nchini humo.
Polisi walimkamata mwanamke huyo pamoja na mwandishi wa habari Mohamed Bashir Hashi, aliyemhoji pamoja na mkuu wa idhaa ya Redio Shabelle Abdulmalik Yusuf.
Hakuna hata mshukiwa mmoja, aliyetuhumiwa amechukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo serikali ya Somalia imesema kuwa ubakaji na dhuluma dhidi ya wanawake ni mambo ambayo hayaruhusiwi hata kidogo, ingawa haikutamka chochote kuhusiana na kesi hii.

Source BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment