Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, November 16, 2013

ZITTO AWASHITAKI WANAO MCHAFUA KUPITIA "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe".


Mh. Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali aliyasema haya "Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe".
Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM.
Wahusika waendelee kuhamisha chanzo lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa mahakamani.
Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa kunichafua kwa tuhuma za uongo. Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa."

No comments:

Post a Comment