Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 22, 2013

ZITTO KABWE NA KITILA MKUMBO WAVULIWA VYEO VYOTE NDANI YA CHADEMA...,

Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.

Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.
 
Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.
 
Tunawapongeza kamati kuu kwa hatua hii muhimu kwa mustakbali wa chama na taifa

No comments:

Post a Comment