Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, December 31, 2013

HIZI NI SHUKRANI ZA DHATI, ZAWADI ZA BARAKA ZILIZOTOLEWA NA MTANDAO WA KING JOFA.

Habari zenu ndugu, jamaa na marafiki na wale woote waliokuwa wakiutembelea mtandao huu wa www.kingjofa.blogspot.com "Kilimanjaro Official Blog"?

Nawashukuru sana kwa muda wenu na kwa mchango wenu mkubwa wa mawazo na pia ushirikiano mkubwa mliouonesha kwa kipindi chote cha mwaka 2013. Na nitakuwa ni mchoyo wa fadhila kama nitashindwa kutoa shukrani zetu za dhati kwa mashabiki wangu wote popote mlipo. Kiukweli mmekuwa faraja kubwa sana kwengu na kwa timu nzima ya KingJofa.
Nachukua nafasi hii kuwatakieni maandalizi mema ya kuupokea mwaka 2014. Na kila lililokuwa gumu kwa mwaka 2013 likawe jepesi katika mwaka 2014. Changamoto mlizozipitia katika mwaka 2013 yakawe mafanikio kwa mwaka 2014. Mpokee baraka na mafanikio tele katika mwaka 2014.
Tunategemea ushirikiano wenu wa hali na mali ili kuhakikisha mtandao huu wa KingJofa unaendelea kufanya vyema siku zote. Maana lengo ni kuwafikishia habari na matukio yenye tija katika jamii na siku zote nitajitahidi kuwapa habari zilizo hakikiwa na kuhaririwa kwa umahiri mkubwa sana.

Mungu Wabariki Ndugu, Jamaa na Marafiki Wooote.
Uendelee kutujalia Hekima, busara na Maarifa yooote,
Usisahau Kuzibariki Kazi Za Mikono yetu wooote, 
Uzidi kuibariki Tanzania, Africa na Dunia yooote.

No comments:

Post a Comment