Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, March 8, 2014

JAMBO SQUAD NA MECCA CHEKA WAMALIZA TOFAUTI ZAO NDANI YA STUDIO ZA NOIZMEKAH

Wasanii wa Arusha wanaotoka katika familia moja maarufu kama "watoto wa bibi" lakini ndani yao kuna makundi tofauti tofauti kama Jambo Squad, MeccaCheka na makundi mengine mengi. Lakini siku za nyuma makundi haya mawili Jambo Squad, MeccaCheka waliingia katika tofauti zinazosemekana ni kushindwa kuelewana kati ya Ordinary wa Jambo squard na Almando Mwerora wa MeccaCheka, ambapo ugomvi huo ulitokea katika studio za Noizmekah zilizopo maeneo ya sakina jijini Arusha. 

Lakini kwa sasa makundi hayo mawili (Jambo Squad na MeccaCheka) wameweza kuzimaliza tofauti zao  zilizokuwepo tokea mwanzo, ambapo kwa mujibu wa wasanii hao waliweza kukutana siku ya Jumatano tarehe 26 Februari 2014 "tulikutanishwa Noizmekah kujadili tofauti zetu, sasa Tumepatana na hakuna beef tena. Shukrani kwa mashabiki zetu wote tunawapenda, tegemeeni ngoma za pamoja toka kwetu Jambo Squad na MeccaCheka kama ishara ya amani na upendo kati yetu vijana, wasanii wa Tanzania, Peace & Love TAZAMA" 
Kutoka kulia ni Ordinary wa Jambo squad, Almando Mwerora, Almando RizChafu, DX ambaye ni producer wa Noizmekah, na Nigga C wa Jambo squad.

Unaweza kutazama Video ya Jambo Squad na MeccaCheka

No comments:

Post a Comment