Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, March 26, 2014

JOHN KESSY AFANIKIWA KUWALIPIA ADA WATOTO ZAIDI YA 27 KUPITIA KILIMANJARO MARATHON 2014

 John Kessy (aliyevaa Tshirt nyekundu) akiwa na rafiki yake kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon.

John Kessy (Tshirt nyekundu) akifurahi baada ya kumaliza kilometa 42 na kukabidhiwa medali

Tshirt zinazouzwa na John Kessy kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu.

 John Kessy akiwakabidhi wanafunzi pesa ili waweze kulipa ada.

 Wanafunzi wakifurahia baada ya kukabidhiwa pesa ya kulipa pesa ya kulipa ada na John Kessy.
Wanafunzi wakilipa ada kwa mwalimu wao.

 John Kessy akiwa amesimama na baadhi ya watoto aliofanikiwa kuwalipia ada.

MOSHI kwa takribani miaka kumi na mbili imezoeleka kuwa kila mwezi wa february au March katika uwanja wa ushirika mkoa wa Kilimanjaro hufanyika mashindano ya kukimbia maarufu kama “Kilimanjaro Marathon”  na watu kutoka mataifa mbalimbali duniani hushiriki katika mbio hizo. Mbio hizo ambazo zimegawanyika katika makundi manne ambayo ni “FULL MARATHON” ambayo ni kilimeta 42, “HALF MARATHON” ambayo ni kilometa 21, “RUN FOR FUN” ambayo ni kilometa 5, na “SPECIAL MARATHON” ambayo ni kwa ajili ya walemavu wa viungo ambao hutumia  “wheel chair” hukimbia kilometa 10.

Kwa kutumia fursa ya mbio za “Kilimanajaro marathon” John Kessy ambaye ni mkazi wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro amae ni afisa maeendeleo ya jamii hususani katika kundi la vijana na watoto, pia ni mwanasosholojia wa kijamii katika nyanja ya elimu, afya na haki za watoto na vijana.  John amekuwa akishiriki katika mbio za “Kilimanjaro marathon” kwa zaidi ya mara sita ambapo alikua akikimbia “HALF MARATHON” lakini mwaka huu aliamua kukimbia “FULL MARATHON” kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia kuwalipia ada na sare watoto wa shule za msingi zilizopo katika manispaa ya Moshi wanaoishi katika mazingira magumu.  

Kauli mbio ya mpango huu wa kusaidia elimu ya watoto ilikuwa ni "RUN FOR A PURPOSE”  yaani “KIMBIA KWA MALENGO” na “ONE KILOMETER ONE KID IN SCHOOL” yaani “KILA KILOMETA MOJA ATAKAYOKIMBIA JOHN KESSY MTOTO MMOJA ATAKUA AMEWEZESHWA KUENDELEA NA SHULE”  Lengo la John Kessy lilikuwa kukusanya zaidi ya fedha za kitanzania milioni tatu na laki sita (3,600,000/=)  kutoka kwa wasamaria mbalimbali ili kufanikisha lengo hilo ambapo kila mtoto angetumia kiasi cha shilingi elfu dhemanini na tano (85,000/=)  kwa kulipa ada na sare za shule.

Hadi kufikia leo tarehe 26 March 2014 John Kessy amefanikiwa kukusanya  jumla ya fedha ya kitanzania milioni mbili na laki tano. Na tayari baadhi ya watoto wameanza kulipiwa ada pamoja na kupata sare mpya za shule watoto zaidi ya ishirini na saba (27). Na John anasisitiza kuwa bado nafasi ipo wazi kwa yeyote atakaeguswa na lengo hili la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Pia kuna Tshirts nzuri ambazo upande wa mbele zimeandikwa “ONE KILOMETER ONE KID IN SCHOOL” na upande wa nyuma zimeandikwa  “RUN FOR A PURPOSE” ambazo kama utanunua  Tshirt hizo utakuwa umesaidia lengo hili la kuwasaidi hawa watoto. Na ikumbukwe  kwamba watoto hawa wanaosaidiwa ni watoto wanaishi katika mazingira magumu.

Wasiliana na John Kessy kupitia namba hizi hapa:- 
+255 (0)782 090 699  au  +255 (0)754 090 699.No comments:

Post a Comment