Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 3, 2014

PANONE AND CO. LTD YASHIRIKI KILI MARATHON KWA AINA YA KIPEKEE

Mbio za kilimanjaro Marathon zilitimua vumbi hapo jana katika mji wa Moshi. mbio za Kili marathon kwa mwaka huu zilibeba washiriki toka nchi zaidi ya Arobaini waliokuja kushiriki mbio hizo za kimataifa.


 Mamia ya wakimbiaji wakiwa wanamaliza mbio za kilometa tano za vodacom.


Hawa ni baadhi ya watu walioshiriki mbio za kilimeta tano "Fun run" wakiwa katika magari yaliyokuwa yamebeba zawadi kwaajili ya washiriki waliofanikiwa kumaliza mbio hizo.

Katika mbio hizo Makampuni mbalimbali yalijitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Katika jambo ambalo lilikua la Kuvutia ni Aina ya Ushiriki wa Kampuni ya Panone katika mashindano hayo.
 Watoto wa kituo cha salama centre wakiwa wamepozi karibu na banda la Panone wakipiga picha ya pamoja na walimu wao baada ya kumaliza mbio salama

Baada ya kuona watoto wamepata fursa ya kuweza kushiriki mbio hizo hasa katika mbio fupi zinazojulikana kama Vodacom Fun run. Panone iliweza kudhamini watoto Takribani HAmsini kutoka katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Salama Centre kilichopo Majengo. Panone iliweza kuwalipia namba za Ushiriki, Kuwatengenezea Tisheti ambazo zilikua na ujumbe ambao ulichaguliwa na watoto hao {Let's Kid's  Run for Fun} na pia kuhakikisha wanashiriki vyema mbio hizo mpaka wanapomaliza na kurudi kituoni salama. Afisa masoko wa Panone and co.ltd ndugu Frank Mwaikatale akizungumza na waandishi wa habari lengo la kampuni yao kudhamini watoto katika mbio hizo

Akizungumza kuhusu Tukio hilo Afisa Masoko wa Panone ndugu Frank Mwaikatale alisema hii ni Fursa kwa jamii kuweza kuiga mfano kwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji katika jamii na Pia kampuni ya Panone inafikiria njia sahihi ya kuwasaidia watoto hao hiyo ikiwa ni moja ya mipango ya kampuni ya kuisaidia jamii. Alimaliza Afisa Masoko huyo kutoka kampuni ya Panone inayosifika katika Uuzaji na Usambazaji wa Mafuta ya Jumla na Rejareja huku wakiwa na Vituo vya uuzwaji wa mafuta katika maeneo mengi Tanzania na Pia kwa sasa kampuni hiyo ina Hotel za kisasa ambapo Hotel moja ipo pale Arusha Sakina kwa idi inayoitwa PANONE GARDEN HOTEL  na nyingine ikiwa pale King'ori kilometa chache kutoka Uwanja wa ndege wa KIA hotel hiyo inaitwa PANONE LUXURY MOTEL


Upendo Person Akipokea zawadi za watoto toka Panone Supermarket zikikabidhiwa na Afisa masoko wa Kampuni hiyo ndugu Frank Mwaikatale.

Huu ni uati wa watu waliofika uwanja wa ushirika kushuhudia kili marathon. 


 Baadhi ya washiriki wa mbio za "Fun run" Baadhi ya washiriki wa kili marathoni kilometa 21 wakimalizia mbio. 


 


Joh makini kutoka weusi kampuni akipagawisha umati mkubwa katika kukamilisha furaha ya kili marathon

Kwenye mopja na mbili alikuwa DJ Drill (Tisheti nyeusi) na Daz Knowledge (Tisheti nyeupe)

No comments:

Post a Comment