Jalala lililopo Kibaoni Linalolalamikiwa na wakazi wa eneo hilo.
WAKAZI wanaoishi mtaa wa Kibaoni
Boman'gombe wilayani hai mkoani Kilimanjaro wameelezea kero na madhara wanayoyapata kutokana na jalala lililopo karibu na makazi ya watu kuwa kero na hatari kwa afya zao.
Wakizungumza
na muandishi wetu ambaye alifika eneo hilo leo majira ya mchana kuhusu kero ya jalala hilo ambalo linaweza kuzusha magojwa mbali
mbali ikiwamo kipindu pindu na majonjwa ya
mlipuko.
Wakazi wa eneo hilo walisema wanapata shida kutokana na harufu mbaya kutokana na
mvua kunyesha pia inzi wamekuwa wengi, pamoja na moshi unaotoka kwenye jalala hilo ambao
usababisha majonjwa ya kukohoa kila wakati.
Mkazi
mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa harufu mbaya kuzagaa kwa takataka hasa mifuko ya rambo na inzi hulazimika kula
chakula uku wakiwa wamefunga milango na madirisha.
"Tunapata
shida sana hasa kipindi hichi cha mvua za masika harufu kali hutoka kwa
wingi na inzi wengi wanafumuka jambo ambalo ni hatari kwa afya zetu
tunaomba Halmashauri watafute shehemu nyingine ya kumwaga taka mbali na
makazi ya watu"
Nae
mkazi mwingine alisema kuwa >> "Wanaoathirika zaidi ni watoto ambao ni
rahisi kupata majonjwa dawa wanazopulizia kwenye maeneo wanayoishi kwa
ajili ya kuua inzi haikidhi maitaji kwani huwa wanarudi baada ya muda
mfupi"
Diwani
wa Kata hiyo ya Hai Mjini Jafar Kiure alisema kuwa wameshapeleka
malalamiko hayo
kwa Mkurungenzi Melzedeck Humbe lakini hadi sasa jambo hilo halija
shudhulikiwa ambapo aliwataka waandishi wa habari kumuuliza Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Clement Kwayu kuhusu jambo hilo.
Akizungumza
jambo hilo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Clement Kwayu alisema kuwa
yupo safarini Tanga pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri na kwamba jambo
hilo watalishudhulikia ili kutatua kero hiyo ili wananchi waishi kwa
amani.
No comments:
Post a Comment