Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, May 13, 2014

TAZAMA PICHA ZA MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WATU...,

Wahitimu Saba wa Shule ya Sekondari ya WATU wakiwa wamekaa kwa furaha katika mahafali yao.


 Wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wakifuatilia Sherehe za maafali.

Mzazi akifuatilia mahafali ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya WATU


Baadhi ya Wageni wakifuatilia Matukio katika Mahafali.


Mkurugenzi mtendaji wa Shule ya Sekondari ya WATU ndugu Josiah Mchome akizungumza katika Mahafali hayo.


 Mwalimu wa Shule ya WATU akitoa zawadi ya Cake kwa wahitimu.


 Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Mobisol ndugu Allan Demol akiwatunuku vyeti Wahitimu.


Watendaji wa Kampuni ya Mobisol wakitoa maelezo ya Huduma zao katika Mahafali hayo.


Mgeni Rasmi Ndugu Allan Demol akiwa Katika Picha na Mmoja wa Wahitimu baada ya kumtunuku Cheti.


Mgeni Rasmi akipokea Kipeperushi toka kwa Mfanyakazi wa Mobisol cha maelezo ya bidhaa zao.

Mgeni Rasmi akitoka kuelekea katika ukumbi wa chakula baada ya Mahafali.

Mgeni Rasmi akiteta jambo na wageni waalikwa nje ya ukumbi

Mkurugenzi mtendaji wa Sekondari ya WATU akikaribisha wageni kwa chakula.

Mgeni akipata chakula cha mchana katika mahafali ya kidato cha sita.


Mgeni rasmi akipata chakula cha mchana


Odran Tarimo kijana aliyesaidia kutimiza ndoto za shule ya WATU akipata chakula.


Odran Tarimo akilishwa keki na mmoja wa wahitimu.Mgeni Rasmi, Walimu nauongozi wa shule wakiwa katika picha ya Pamoja na Wahitimu. 

Shule ya Sekondari ya WATU iliyopo katika kata Ya Karanga Wilayani ya Moshi mjini ni Moja ya Shule ambazo zipo katika Hatua nzuri kwa sasa. Shule hii ya WATU ni shule ambayo imeanzishwa kwa lengo la kusaidia wanafunzi ambao wana ndoto ya kupata elimu bora lakini wanakwamishwa na Hali ngumu ya uchumi wa familia zao na kupelekea familia kushindwa kuwalipia Mahitaji yao muhimu ya shule kama Ada, Vitabu, Daftari nk.

Akizungumza katika Mahafali ya Kwanza ya Kidato cha Sitayaliyofanyika jana katika Shule hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Shule ya watu Ndugu Josiah Mchome alitangulia kuelezea historia ya shule hiyo ambayo iliweza kusisimua wageni mbalimbali na kuweza kushangazwa na Jitihada zake alizozionesha katika kufanikisha wazo lake ambalo alilifanyia kazi kwa zaidi ya Miaka nane huku akifanya kazi kwa kujitolea bila kupata mshahara.

Akimtaja kijana ambaye alikua nae bega kwa bega katika kipindi hicho ndugu Odrian Tarimo. Alitumia mifano kuwapa vijana waliohitimu hapo jinsi Odrian alivyojitolea kwa zaidi ya miaka mitano bila kupata mshahara mpaka kufikia mafanikio ya shule hiyo.

Hata hivyo Ndugu Mchome alitoa Shukrani kwa wafadhili waliojitolea na wanaoendelea kujitolea kusaidia shule hiyo na kusema anafuraha kuona Taifa linasaidiwa kwa kutoa elimu kwa vijana kupitia shule hiyo ya WATU iliyo chini ya Taasisi ambayo ilisajiliwa kama NGO yenye lengo la kuhamasisha watu washiriki katika kupata elimu na ndipo mwishowe likazaliwa wazo la kuwa na shule baada ya kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo kugundua jamii kubwa inahitaji elimu na haina uwezo wa kuipata.

Hata hivyo Ndugu Odran Tarimo alipata fursa ya kuzungumza na kuelezea changamoto walizokumbana nazo katika safari yao ya ndoto ambayo leo imetimia huku akiwasihi vijana hao kuwa na moyo wa kujitolea.

Shule ya watu ambayo katika matokeo ya awali ya kidato cha Sita imeweza kushika nafasi ya pili katika kanda ya kaskazini huku ikiongoza mkoa wa kilimanjaro hiyo ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa ya shule hiyo.

Ndugu Allan Demol ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mobisol ambaye alikua mgeni Rasmi katika mahafali ya kuwatunuku wanafunzi saba waliohitimu elimu ya kidato cha sita katika shule hiyo alitoa sifa nyingi kwa shule hiyo huku akitoa zawadi ya Sola ya kisasa ya kuchaji simu kwa Shule hiyo pamoja na Kuwafungia Wireless Network katika shule hiyo. Hata hivyo Kampuni ya Mobisol ndiyo moja ya chachu ya mafanikio ya shule hiyo iliyo katika eneo ambalo halina umeme na kuwezesha kufunga sola katika shule hiyo na wanafunzi kupata elimu chini ya mwanga wa Sola ambao ulitenganisha shule hiyo na kiza. Ndugu Allan aliwasihi wanafunzi hao kutumia elimu yao kam njia ya kupata elimu zaidi na kuwasihi kuwa na vitu vya ziada ili kukabiliana na Suala la Ajira katika Jamii yao.


No comments:

Post a Comment