Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 18, 2014

HALMASHAURI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUUNDA KAMATI ZA USIMAMIZI WA ARDHI

Halmashauri zote nchini zimeagizwa kuunda kamati za usimamizi wa ardhi na mazingira katika ngazi ya wilaya na vijiji ambazo zitafanyakazi kwa kushirikiana na wananchi katika swala zima la utunzaji na ulinzi wa mazingira katika maeneo yao.

Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais mazingira Mh. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya kupambana na kuenea kwa jangwa duniani, iliyofanyika kitaifa katika kijiji cha mabilioni wilayani Same mkoani Kilimanjaro na kusema kuwa wananchi hawanabudi kushirikishwa katika kuyalinda na kuyatunza mazingira.

Aidha ,Mh Mwalimu amewataka viongozi kuacha tabia ya kukaa kwenye mikutano na vikao vya wataalamu na watendaji na kutumia fedha zilizotengwa kwajili ya miradi ya utunzaji wa mazingira na badala yake fedha hizo zipelekwa vijijini kwa wananchi, ili zitumike katika kutunza mazingira
Awali akisoma taarifa ya katika maadhimisho hayo.

Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais Julius Ningu amesema asilimia 61 ya baadhi ya maeneo katika mikoa saba ya Tanzania yako hatarini kugeuka jangwa hivyo serikali kupitia mfuko wa hifadhi ya mazingira kwa kushirikiana na mfuko wa maendeleo duniani (undp) umeanzisha miradi ya kuhifadhi mazingira.

Akitoa taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Bw Leonidas Gama,mkuu wa wilaya ya Same Herman kapufi ameseama, mkoa huo unatarajia kulotesha miti milioni 11 kwa kipindi cha 2014 ,huku mwenyekiti wa kamati yautekelezaji wa matumizi wa endelevu ya ardhi SLM mkoani Kilimanjaro Bw. Pauli shayo ,akielezea mafanikiyo ya mradi huo.

No comments:

Post a Comment