Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 17, 2014

WATU WAWILI WAKUTWA WAMEKUFA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI

KILIMANJARO wananchi wameokota mabaki ya mwili wa binadamu ambaye amafariki muda mrefu kakika kijiji cha Sofe kata ya kilomeni wilayani mwanga mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa polisi mkoa ni Kilimanjaro Bwana Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio la kuokotwa kwa mabaki ya mwili siku ya jumatano tarehe 16 Julai mwaka huu majira ya saa 4:00 asubui katika vichaka vilivyopo katika kijiji hicho, na kwamba alitambuliwa kwa jina la Christian Malacha (45) ambae alikuwa amapotea nyumbani kwa muda mrefu.

Katika tukio lingine Kamanda Boaz alisema wananchi wa kijiji cha Rau River wilaya ya  moshi mkoani Kilimanjaro waliokota mwili wa mtu mwingine aliyefahamika kwa jina la Manase Lyatuu (51) fundi ujenzi mkazi wa kijiji cha Kalala, ambapo maiti hiyo imeonekana na jeraha kubwa kichwani na mdomoni.

Kamanda alisema maiti hiyo iliokotwa katika shamba la Raphael Kaloki, na kwamba uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini chanzo cha kifo cha marehemu huyo.

No comments:

Post a Comment