Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 17, 2014

KAYA MASKINI ZILIZOPO KATIKA VIJIJI SITINI WILAYANI SAME KUNUFAIKA NA MFUKO WA TASAF

KILIMANJARO kaya maskini zilizopo katika vijiji sitini wilayani Same mkoani Kilimanjaro zitanufaika na mpango wa waserikali wa kunusuru kaya hizo katika utekelezaji wa awamu ya tatu ya  mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika, sekta ya afya , elimu ya msingi na sekondari

Akionge katika  warsha maalumu ya uzinduzi wa TASAF awamu ya tatu, iliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo meneja rasilimali watu wa makao makuu ya TASAF Bi. Tekla Makundi alisema zaidi ya watu elfu nane na mia tisa (8,900)  watanufaika na mpango huo katika vijiji vilivyopo wilayani Same.

Mratibu wa  TASAF wilayani Same Bi. Tumaini Lyatuu aliseama mpango huo katika awamu ya pili ulikuwa na changamoto mbalimbali zilizo sababisha kutofanikiwa kwa mradi huo kutokana na wananchi kushindwa kuchangia asilimia 20, hivyo watatoa elimu ya kutosha wananchi watambue umuhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo.

Akizindua utekelezaji wa mpango huo mkuuu wa wilaya hya Same Bw. Herman Kapufi  aliwaonya viongozi wa serikali za vijiji  na wawezeshaji watakao hujumu mpango huo watachukuliwa hatua kali za kisheria kama walivyo chukuliwa baadhi ya viongozi waliochakachua mradi huo katika awamu ya pili.

No comments:

Post a Comment