Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 8, 2014

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UKATILI KWA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI

KILIMANJARO mkazi mmoja wa Singida mjini aliyefahamika kwa jina la Jackline Kweka (30) jana alipandishwa Mahakama ya wilaya ya Hai akikabiliwa na tuhuma za kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani mwenye umri wa miaka 15.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akimpiga mfanyakazi wake huyo sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo kumvuta nyama za siri kwa kutumia plaizi.

Baada ya tuhuma hizo kuibuliwa na raia wema mtuhumiwa huyo alitoroka kutoka mkoani Singida na kukimbilia katika kijiji cha Narumu wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro alikokamatiwa baada ya taarifa kuvuja.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani mbele ya hakimu mkazi, mfawidhi wa wilaya, Denis Mpelembwa na kukanusha mashitaka dhidi yake. Hati ya mashitaka hayo ni ya awali ili kuruhusu polisi kutoka Singida kwenda kumchukua mtuhumiwa huyo.

Akisoma mashitaka Mwendesha Mashitaka wa polisi, inspekta Marwa Mwita alidai mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo Julai mwaka 2014, kwa siku tofauti tofauti.

Mtuhumiwa huyo alikanusha mashitaka hayo na amerudishwa rumande hadi Agosti 21 mwaka 2014, wakati ukisubiriwa utaratibu wa kumsafirisha kwenda mkoani Singida.

Msichana anayedaiwa kufanyiwa ukatili huo alilazwa katika hospitali ya wilaya ya Hai kwa Matibabu na taarifa zinadai amepoteza uwezo wa kusikia na hapati tene siku zake za hedhi.

No comments:

Post a Comment