Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 8, 2014

KESI YA MAREHEMU MTOTO "NASRA RASHID MVUNGI" YAPIGWA TENA TAREHE

Kutoka kushoto ni aliyekuwa mlezi wa marehemu mtoto Nasra Rashid, Bi. Mariam Said  baba yake na Nasra, Bw. Rashid Mvungi na mume wa Bi. Mariam Said, Bwana Mtonga Omary.

Watuhumiwa Bw. Rashid Mvungi pamoja na waliokuwa walezi wake, Bi. Mariam Said na mumewe Mtonga Omary, wakiwa mahakamani.


Umati wa watu waliokuja kusikiliza kesi ya marehemu mtoto Nasra, wakiwa nje ya mahakama.

MOROGORO washtakiwa watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji dhidi ya mtoto Nasra Rashid Mvungi, wamelazimika kubadilishiwa hakimu baada ya hakimu ambaye kesi yao imekuwa ikifikishwa mbele yake kwaajili ya kutajwa, kupata dharura na kutokuwepo mahakamani hapo.

Washtakiwa hao ambao kesi yao imekuwa ikifikishwa na kutajwa, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, Mary Moyo,  wamelazimika kupandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Agripina Kimanze na kusomewa mashtaka yao, baada ya hakimu Moyo kutokuwepo mahakamani hapo.

Kufuatia hali hiyo, washtakiwa hao walichelewa kupanda kizimbani tofauti na nyakati nyingine, hali iliyoonekana huenda ilisababishwa na mabadiliko hayo ya kukosekana kwa hakimu husika.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Aminatha Mazengo, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba jalada bado lipo kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali, hivyo kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Mahakama imeridhia ombi hilo, na kupanga Agosti 20 mwaka 2014, kufikishwa tena kwa kesi hiyo kwaajili ya kutajwa, kutokana na mahakama hiyo kukosa uwezo kisheria kusikiliza shtaka la mauaji  huku washtakiwa wakirudishwa rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo ya mauaji inawakabili washtakiwa watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto Nasra, Bw. Rashid Mvungi pamoja na waliokuwa walezi wake, Bi. Mariam Said Na mumewe Mtonga Omary, ambao awali walikuwa wakikabiliwa na shtaka la kula njama na kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya Mtoto Nasra Mvungi kabla ya baadaye mashtaka yao kubadilishwa na kuwa ya mauaji baada ya mtoto huyo kufariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment