Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 19, 2014

MAJAMBAZI WAMUUA MLINZI KIKATILI NA KUPORA MALI

MOSHI  watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamempiga mlinzi wa jengo la  Lyamuya Constraction, Musa Muhamed (52) mkazi wa Mabogini, na kitu kibutu kichwani na kusababishia kufariki dunia, pamoja na kuvunja maduka mawili yaliyopo katika jengo hilo la Lyamuya Constraction.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea usiku wa kuamkia agusti 18  mwaka 2014 , katika mtaa wa kaunda, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambapo watu hao waliingia katika jengo hilo na kumpiga mlizi huyo na kitu kizito kichwani.

Boaz alisema baada ya kumpiga mlizi huyo watu hao walim'buruta hadi sehemu ambapo magari ya jengo hilo huegeshwa na kuutelekeza mwili wa marehemu.

Alisema watu hao baada ya kufanya unyama huo walivunja maduka  mawili  ambapo waliiba tarakilishi “Computer” mbili na vitu mbalimbali ambavyo thamani yake hajaweza kufahamika kwa haraka.

Kamanda Boaz, alisema walivunja duka la mimea na mifugo na kuiba tarakilishi “Computer” na vitu vingine ambavyo havija tambuliwa na wahusika ambapo alisema pia walivunja duka la vifaa vya umeme ambapo pia waliiba tarakilishi “Computer” na vifaa mbalimbali vya umeme.

Boaz alisema hakuna anaeshikiliwa hadi sasa na kwamba uchunguzi unaendelea ili  kuweza kuwatia nguvuni waliofanya tukio hilo, na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi.

No comments:

Post a Comment