Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 15, 2014

WANANCHI WALALAMIKIA HUDUMA MBOVU ZA AFYA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA

HAI wananchi wa mtaa wa kibaoni, kata ya  Hai mjini, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamelalamikia utaratibu na huduma zinazotolewa na hosipitali ya wilaya ya Hai kuwa haziridhishi na wananchi hao kulalamikia kudorora kwa huduma muhimu kama ya afya.

Wananchi hao wametoa malalamiko hayo hivi karibuni wakati wa mkutano wa  hadhara uliofanyika katika ofisi ya Mtaa wa Kibaoni na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Hai  Novatus Makunga, pamoja na wakuu wa idara wa wilaya ya Hai,  katika kusikiliza  kero mbalimbali za wananchi.

Baadhi ya kero ambazo wananchi hao walizitoa mbele ya mkuu wa wilaya ni pamoja na lugha chafu kwa baadhi ya wauguzi, muda mrefu wa kusubiri huduma mapokezi pamoja na ukosefu wa dawa tatizo linalo leta kero kwa wagonjwa.

Awali akisoma risala kwa mkuu wa wilaya mwenyekiti wa mtaa wa kibaoni ambaye ni diwani wa viti maalumu Amina Swai,  alisema kuwa  wagonjwa wamekuwa wakikosa dawa hospitalini hapo na kuelekezwa  kununua dawa hizo katika maduka ya dawa yanayomilikiwa na watu binafsi.

Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Felista Ritte, alikiri kuwepo kwa kero hizo hospitalini hapo na kusema kuwa tayari kuna watu na kitengo maalumu cha kusikiliza kero na kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwachukulia sheria kali kwa wauguzi na madaktari watakao kiuka wajibu wao kwa wagonjwa.

Ameongeza kwa kuwataka  wananchi hao kuwa wazalendo wa kuepuka gharama kubwa za kulipia matibabu kwa kuwataka kukata bima ya afya ili kuwarahisishia kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment