Wananchi, watumishi wa umma na mashirika binafsi hapa nchini Tanzania wameshauriwa kujiunga katika vyuo
vikuu huria vilivyopo hapa nchini ili waweze kujiongezea elimu itakayo wawezesha
kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi sambamba na kumudu ushindani wa soko la ajira.
Rai hiyo imetolewa na rais wa wanafunzi wa chuo kikuu huria cha mjini Moshi Bw. Adinani Kingazi ,walipotembelewa chuoni hapo na makamu
mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania Bw. Tolly Mbwette, ambapo amesema jamii
inatakiwa kutambua kuwa ,kuna umuhimu wakujiendeleza kielimu.
Bw. Kingazi alisema njia pekee ambayo itakayoweza kumkomboa
mtumishi wa umma ama sekta binafsi kukabiliana ipasavyo katika soko la ajira
ni kusoma katika chuo kikuu huria, ambapo kinampa fursa ya kusoma bila kuathiri
shughuli zake za kiutendaji.
Makamu mkuu
wa chuo kikuu huria nchini Bw. Tolly Mbwette alisema serikali imeanza kuboresha
baadhi miundombinu ikiwemo majengo katika vyuo vikuu huria hapa nchini pia katika kutekeleza
mpango wa matokeo makubwa sasa ina mpango maalumu wa kuhakikisha kuwa inajenga vyuo vikuu huria nchi nzima.
No comments:
Post a Comment