Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 17, 2014

VIJIJI 120 KATIKA WILAYA 7 MKOANI KILIMANJARO KUNUFAIKA NA UMEMEN WA BURE

KILIMANJARO jumla ya vijiji 120 vya wilaya saba za mkoani Kilimanjaro wanatarajia kunufaika na utekelezaji wa umeme vijijini (REA) ambao unafadhiliwa na serikali na kutekelezwa na shirika la taifa la ugavi wa umeme TANESCO.

Afisa masoko wa tanesco makao makuu bi. Rose Kundecha aliseama serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni  27, kwaajili ya mradi huo ambao umeanza kutekelezwa katika vijiji mbalimbali nchini kwa wataalamu kupima maeneo ya miundombini ya mradi huo.

Bi. Kundecha aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika vijiji  vinne tofauti vilivyoko wilayani Rombo kwa lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya mradi huo kwa kuwa umefadhiliwa naserikali na kwamba wananchi wanatakiwa kuruhusu miundombinu ya mradi huo bila kulipwa fidia.

Mwenyekiti wa kijiji cha manda juu Bi. Amadi Massawe pamoja na kuipongeza serikali kwa kuwapatia umeme katika kijiji hicho lakini pia ameahidi kushirikiana na wananchi katika kulinda  miundombinu ya mradi huo zikiwemo transoma na nyaya za umeme.

 Meneja masoko wa tanesco wa wilaya ya Rombo Bw. Rajabu Haule alisema, pamoja na serikali kutoa ofa ya kusambaza umeme huo kwa mara ya pili lakini bado kuna vijiji vingi ambavyo vinahitaji kusambaziwa umeme.

No comments:

Post a Comment