MOSHI wenyekiti wa vijiji 37 vinavyozunguka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, wamepanga
kumuona waziri wa Maliasili na Misitu, Mhe. Lazaro Nyalandu, ili aweze kuona umuhimu
wa kuwarejeshea wananchi hao eneo la msitu wa Nusu Maili, ili waweze kuulinda
msitu huo usiendelee kuharibiwa kama ambavyo unafanyika sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari, kwa niaba ya Wenyeviti hao, Mwenyekiti wa Mtandao wa vijiji
37, KIHACONE, Boniface Mmbando amesema wananchi hao wamepanga kwenda kumuona waziri Nyalandu, wakimtaka kuwarejeshea msitu huo kwa wananchi kwani wao ndio walinzi wakubwa wa
rasilimali hizo.
Amesema hali ya uharibifu wa mazingira katika wilaya ya Moshi unatisha kutokana
na watu kuendelea kukata miti hovyo, na kwamba kama jitihada za makusudi
hazitachukuliwa kwa haraka kuna hatari kubwa ya kukumbwa na jangwa.
Mmbando amesema lengo la kuanzishwa kwa Mtandao huo ni kudhibiti hali ya
uhalibifu wa mazingira ambao unafanyika ndani ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, lakini
wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na vitisho ambavyo wamekuwa
wakivipata kutoka kwa KINAPA.
No comments:
Post a Comment