Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 29, 2014

Manispaa ya Moshi, jiji la Arusha na Dar es Salaam kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Uhifadhi wa Mazingira

Halmashauri ya manispaa ya Moshi, jiji la Arusha na jiji la Dar es salaam zimechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya uhifadhi wa mazingira kwa mwaka 2015-2016.  

Hayo yamebainishwa na mratibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira (WWF) Dr Teresia Olemako, wakati wa semina maalumu kwa wakuu wa idara wa halmashauri ya manispaa ya Moshi iliyofanyika mjini Moshi ambapo alisema kwa mwaka huu Tanzania itashiriki kwenye majaribio.

Alisema pamoja na kwamba mashindano hayo yana husu majiji, manispaa ya Moshi imetajwa kuwa ni mdau mkubwa katika kushiriki kutokana na juudi zake za muda mrefu za kutunza mazingira na kuweza kukabiliana, hivyo semina hiyo ni kwajili ya kuwaanda wananchi wa halmashauri hiyo jinsi ya kushiriki .

Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Shabani Ntarambe alisema manispaa hiyo tayari ipo kwenye rekodi ya dunia kutokana na kufanya vizuri katika swala la uhifadhi wa mazingira ukiwemo mlima Kilimanjaro.

Nae mbunge wa manispaa ya moshi Philemon Ndesamburo, amewataka wananchi wa manispaa hiyo kutumia nafasi hiyo katika kuongeza kasi ya utunzaji wa mazingir ili Tanzania iendelee kupeperusha bendera kimataifa katika swala la utunzaji wa mazingira.

No comments:

Post a Comment