Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 27, 2014

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM awataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM, Agrey Marealle, amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

 Akizungumza katika  mkutano wa umoja wa vijana wa wilaya ya Moshi mjini, uliofanyika katika kata ya Pasua Manispaa  ya  Moshi Mkoani Kilimanjaro,  Marealle amesema kuwa  ni wakati wa vijana kutumia fursa  zilizopo ikiwa ni pamoja na uchaguzi huo  kwa  kushiriki chaguzi mbali mbali na kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.



Marealle amewataka watanzania kuendelea kuidumisha tunu ya nchi ili kusiwepo na machafuko  ya umwagaji damu kutokana na baadhi ya vijana wamekuwa wakihamasihwa kujitokeza katika maandamano na kusababisha kuwepo kwa uvunjifu wa amani.

Kwa upande wake katibu wa vijana CCM, wilaya ya Moshi Mjini, Joel Makwaiya amesema kumekuwepo na viendo vya kufanyiwa vurugu na baadhi ya wafuasi wa vyama pinzani pindi mikutano hiyo ya CCM inapofanyika.
Nae Mwenyekiti wa vijana CCM, wilaya ya Moshi, Abdallah Thabiti amewataka vijana na wananchi kutokubali kurubuniwa na wanasiasa kutoka nje ya CCM, jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani.

Hata hivyo Mmoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani hapa,  Ngangange mtenga, amewataka vijana, hususan wajasiriamali, kuacha tabia ya ubinafsi,  badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kupata fursa za kimaendeleo na kupatiwa mikopo kwa urahisi.

Mtenga aliongeza kuwa sifa ya sirikali ni kupeleka maendeleo kwa wananchi wake hivyo akatumia fursa hiyo kuwataka vijana hao kuondokana na dhana ya kuwa vibaraka wa kutumiwa na vyama vya upinzania kuwa vitawaletea maendeleo.

Mkutano huo pia , mjumbe wa Nec, alimsimika Edmund Rutaraka kuwa Naibu kamanda wa vijana wilaya ya moshi mjini, ambapo amewaomba vjana hao kumpa ushirikiano katika kukiimarisha chama hicho.

Katika mkutano huo,  wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema walifika wakiwa na gari aina ya Noah kwa lengo la  kuvuruga mkutano huo, hata hivyo walidhibitiwa na askari waliokuwepo katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment