Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 23, 2014

Mbunge wa Njombe akabidhi milioni mbili kusaidia maendeleo ya shule katika jimbo lake

Naibu waziri wa ujenzi Mhandisi Gerison Lwenge,  ambae pia ni mbunge wa jimbo la Njombe Magharibi amekabidhi kiasi cha shilingi milioni mbili  kwa ajili ya kuendesha shule pamoja na  vitabu arobaini na tisa (49) vya masomo mbalimbali  vikiwemo  vya  sayansi katika shule ya sekondari ya luduga iliyoko wilayani wanging’ombe .

Akiwa katika ziara ya siku kumi na nne wilayani wanging’ombe   mhandisi Lwenge  alisema kwa kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini imemlazimu kupeleka vitabu hivyo katika shule   zote  za sekondari zilizopo katika jimbo lake ili wanafunzi waweze kujisomea na kuleta ufaulu mkubwa katika masomo ya sayansi.

Aidha mhandisi  Lwenge  alisema katika  mchakato wa rasimu ya katiba serikali imepitisha kipengere cha elimu ya msingi kweda hadi kidato cha nne ambapo itakuwa na mitaala ya masomo mbalimbali yakiwamo ya ufundi stadi na kilimo yanayowapa  wanafunzi fursa ya kujitegemea wanapohitimu  elimu hiyo. 

Katika hatua nyingine mhandisi Lwenge aliwahakikishia wananchi wa vijiji vya kata ya Luduge na vijiji vya Korinto, Kilonge na Mwambegu kupelekewa miundo mbinu ukiwemo umeme mwaka  huu ambapo vijiji vingine vitapatiwa kwa awamu nyingine itakayofuata, nakuwataka wananchi  watakao wekewa umeme  kwa awamu hii kuweka maandalizi kwa ajili ya umeme huo.

Akisoma taarifa fupi ya shule hiyo mkuu wa shule ya Luduga alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji, upungufu wa nyumba za waalimu, mabweni, bwalo la chakula pamoja na maabara za kisasa.

No comments:

Post a Comment