Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 23, 2014

Mratibu wa elimu awahamisha wanafunzi 29 bila ridhaa ya wazazi na walezi

Baadhi ya wazazi na walezi mkoani Njombe  ambao watoto wao walikuwa wanasoma katika kituo cha chekechea na awali  Ihungilo wamelalamikia kitendo cha mratibu elimu kata ya Ihungilo,  Bwana Lugumko Kienga kwa kuwahamisha watoto  wao kutoka  kituo hicho na kuwapeleka  katika shule ya awali iliyopo katika shule ya msingi Ihungilo.

Wakiongea kwenye  mkutano wa wazazi na bodi ya kituo hicho uliofanyika kituoni hapo walisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha mratibu huyo  cha kuwahamisha watoto wao bila ya ridhaa yao.

Akizungumza na wazazi na walezi wa watoto hao  mwenyekiti wa bodi wa kituo hicho Olasi Mkulo alisema idadi ya watoto waliohamishwa kutoka kituo hicho ni watoto ishiri na tisa (29)  ambapo amelaani kitendo hicho na kusema kuwa kitendo alichofanya mratibu huyo hakikufwata utaratibu kwakuwa alitakiwa kukutana na uongozi wa kituo hicho  na kukubaliana.

Kwa upande wa mratibu elimu Bw. Kienga alisema kuwa imemlazimu kuchukua uamuzi huo kwani kituo hicho hakijakidhi vigezo vya kituo cha awali na hakijakamilisha usajili wala hakina vifaa  vyakutosha kwa ajili ya kufundishia.

Kituo  cha chekechea na awali cha ihungilo  kilichopo chini ya parokia ya uliwa  kimeanzishwa mwaka 1998 ambapo hadi sasa takribani watoto thelathini wanasoma katika kituo   hicho.

No comments:

Post a Comment